Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 30 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 386 2025-05-22

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza:-

Je, kwa nini Askari Polisi hawalipwi fedha za likizo?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imekuwa ikitenga fedha kwenye bajeti yake kila mwaka kwa ajili ya malipo ya stahili mbalimbali ikiwa ni pamoja na malipo ya likizo kwa Askari Polisi. Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Jumla ya kiasi cha fedha 4,359,600,000 kimelipwa na katika mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya kiasi cha fedha 4,475,000,000 kimetengwa kwa ajili ya askari kwenda likizo. Serikali itaendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya malipo na stahili mbalimbali za askari ikiwemo malipo ya likizo. Ahsante.