Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza:- Je, kwa nini Askari Polisi hawalipwi fedha za likizo?

Supplementary Question 1

MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Swali la kwanza, ninaomba kujua ni lini Serikali italipa madeni mbalimbali ya Maafisa Polisi na Askari wa vyuo mbalimbali pamoja na Askari Magereza fedha zao wanazozidai?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kwa nyakati tofauti tofauti Serikali imekuwa ikiahidi kwamba, inahakiki madeni yote ya askari hapa nchini, lakini mpaka sasa hakuna majibu yaliyotolewa. Je, ni lini Serikali itamaliza uhakiki wa madeni ya Askari Polisi wote wa Tanzania ikiwa ni pamoja na Askari wetu wa Mkoa wa Mbeya wanajitoa sana kufanya kazi, lakini wanadai fedha kwa muda mrefu?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niwapongeze sana Askari wetu kwa kazi kubwa wanayofanya ya kulinda rai ana mali zao hapa nchini. Pia nimpongeze Mheshimiwa Mbunge Suma Ikenda ambaye amekuwa akiwapambania sana Askari wetu hapa nchini pamoja na Mkoa wa Mbeya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo yangu naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, Mheshimiwa Mbunge anataka kujua je, ni lini malipo yatakamilika kwa Askari Magereza na Polisi? Kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka na kulipa Askari wetu. Kama nilivyojibu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 tayari wameshalipa fedha kiasi cha bilioni 4.3 na kwenye mwaka wa fedha huu unaoendelea 2024/2025 wametenga bilioni 4.7 tayari kwa ajili ya kulipa Askari wetu wa Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kulipa askari polisi hii itaenda sambamba pia na Askari wa Jeshi la Magereza na Askari wengine. Kila mwaka Serikali inatenga fedha kupitia majeshi hayo kwa ajili ya kulipa madeni ya Askari wetu ambao wanafanya kazi kubwa hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, ni kweli Serikali imekuwa ikifanya uhakiki na ndiyo maana tumelipa hawa, baada ya kukamilisha uhakiki ndipo tunafanya malipo. Tunafanya uhakiki, baada ya kumaliza uhakiki tunapeleka Wizara ya Fedha kwa ajili ya malipo. Kwa hiyo, Serikali itafanya hivyo kila wakati kuhakiki madeni na kulipa kama ambavyo nimejibu kwenye jibu la msingi. Ahsante sana.