Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 30 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 387 2025-05-22

Name

Dr. John Danielson Pallangyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:-

Je, lini Serikali itakuja na mpango wa kupima na kupanga makazi yaliyopo kando ya Barabara Kuu ya Moshi - Arusha na Arusha bypass?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Programu ya KKK iliziwezesha Halmashauri za Wilaya za Meru, Moshi na Arusha ambazo zinapitiwa na barabara Kuu ya Moshi – Arusha na barabara ya mchepuko (bypass) kwa kuzipatia fedha kiasi cha shilingi billioni 1.9 ambazo zilitumika kupanga, kupima na kumilikisha jumla ya viwanja 4,160 na hili ni zoezi endelevu kukabiliana na hali hiyo ya ukuaji wa kasi wa miji yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa rai kwa Mamlaka za Upangaji nchini kuendelea kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuainisha maeneo au miji chipukizi ikiwepo ile iliyopo kandokando mwa barabara zetu iliyoiva kwa ajili ya kuendelezwa kama miji kwa mujibu wa Sheria ya Mipangomiji ili maeneo hayo yaweze kupangwa, kupimwa na kumilikishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mamlaka hizo zinashauriwa kuwasilisha andiko Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kuwezeshwa Mikopo kwa ajili ya Miradi hiyo ya Upangaji, Upimaji na Umilikishwaji katika kukabili ukuaji wa Kasi wa Miji yetu.