Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:- Je, lini Serikali itakuja na mpango wa kupima na kupanga makazi yaliyopo kando ya Barabara Kuu ya Moshi - Arusha na Arusha bypass?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi hii tena na nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini niseme tu kwamba, kumekuwa na makampuni mengi sasa hivi ambayo yanafanya biashara ya ardhi kwa sababu ardhi ni mali na mtaji mkubwa. Wanachokifanya ni kununua mashamba na kuyakatakata katika viwanja vidogo vidogo na kuuzia wanaohitaji. Je, Serikali haioni kwamba, sasa hivi ni wakati muafaka wa kutoa mwongozo wa namna gani ya kufanya biashara ya ardhi ili tuondokane na biashara hii kusababisha miji yetu inakuwa ni squatters?
 
											Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
								NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tunayo makampuni mengi ambayo yanafanya shughuli hizi za upimaji wa ardhi yetu hapa nchini, lakini tuna miongozo tayari inayowaelekeza namna ya kufanya kazi zao ili kuondokana na haya maeneo ya squatter. Inawezekana kabisa kukawa na ukiukwaji wa zile taratibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe maelekezo kwa makamishna wasaidizi wa mikoa, makampuni binafsi yatakapojishirikisha kwenye eneo lolote ambalo limebainika basi lazima yale maombi yao yapite kwa makamishna ili kuhakiki ili kusijitokeze tena ujenzi holela kwenye maeneo ya wananchi na hata kuwa na standard za viwanja kwa sababu wanapima viwanja vidogo vidogo square meter 200, square meter 300 wakati mwingine hazileti tija kwenye maeneo yenu.
							
 
											Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:- Je, lini Serikali itakuja na mpango wa kupima na kupanga makazi yaliyopo kando ya Barabara Kuu ya Moshi - Arusha na Arusha bypass?
Supplementary Question 2
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wangu waishio maeneo ya Girafu Bara walitoa fedha zao kwa ajili ya kupimiwa viwanja hivyo, lakini mpaka sasa hivi ni zaidi ya miaka kumi bila kupata hati wala kupimiwa. Je, nini kauli ya Serikali juu ya wananchi wangu waliokaa miaka yote hiyo bila kujua hatma ya kupata hati zao? Ninakushukuru.
 
											Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa wakati mpango huu wa KKK ulipoanza ulijitokeza tatizo kwenye makampuni ambayo yalikuwa yanaendesha zoezi hili na kwa sasa tumekuja na mpango maalum wa ukwamuaji ambao unakwenda kutibu ugonjwa huu wa wananchi waliochukuliwa fedha zao na makampuni ili wapate hati na kumilikishwa maeneo yao. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge tuvute subira kidogo wakati tunalichakata kwa sababu si tatizo la sehemu moja kimsingi ni tatizo la nchi nzima.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved