Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 432 2025-05-28

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kujenga shule ya sekondari Kata ya Kikeo – Mvomero?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikijenga shule mpya za kata kwa ajili ya kupunguza msongamano darasani na watoto kutembea mwendo mrefu. Kupitia mpango huu Kata za Homboza, Kweuma na Mkindo za Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, tayari zimejengewa shule mpya.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2024/2025 Serikali imetenga shilingi milioni 528.99 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kutwa katika Kata ya Kikeo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kujenga shule za kata katika maeneo yenye shule zenye msongamano au maeneo ambayo wanafunzi wanatembea mwendo mrefu kadiri ya upatikanaji wa fedha.