Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 433 2025-05-28

Name

Eric James Shigongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Primary Question

MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: -

Je, Serikali inafahamu tatizo la uhaba wa walimu, hasa wa masomo ya sayansi nchini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inafahamu tatizo la uhaba wa walimu hasa masomo ya sayansi nchini. Sensa ya Elimu Msingi Mwaka 2024 inaonesha kuwa mahitaji ya Walimu wa Masomo ya Sayansi ni 31,123, waliopo ni 21,309 na upungufu ni walimu 9,814.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikiajiri walimu wa kada mbalimbali ikiwemo walimu wa masomo ya sayansi kadiri ya upatikanaji wa fedha. Mwaka 2024/2025 Serikali imeajiri walimu 15,925 wakiwemo walimu wa masomo ya sayansi 5,115 ambao wamepangiwa vituo vya kazi katika maeneo yenye upungufu zaidi. Serikali itaendelea kuajiri walimu wa masomo ya sayansi kadiri ya upatikanaji wa fedha.