Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 434 2025-05-28

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. ASIA A. HALAMGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Kata ya Endagau Jimbo la Hanang?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2024/2025 Serikali imetenga shilingi bilioni 53.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya kwenye kata 214 za kimkakati, ambapo kila kituo kitapokea shilingi milioni 250. Katika Halmashauri ya Hanang, fedha hizo zitapelekwa katika Kata ya Hidet kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Endagau ina jumla ya wananchi 6,286 na iko umbali wa kilometa 8 kutoka Kituo cha karibu cha Endasak.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati na zitakazokidhi vigezo kote nchini, zikiwemo Kata za Halmashauri ya Hanang.