Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 435 2025-05-28

Name

Emmanuel Adamson Mwakasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA K.n.y. MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:-

Je, kuna mkakati gani wa kuondoa upungufu wa vituo vya afya katika Kata za Tabora Mjini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Manispaa ya Tabora ina jumla ya kata 29 ambapo kata tano ndio zina vituo vya afya na Hospitali ya Manispaa. Mwaka 2023/2024 Serikali kupitia mapato ya ndani ya halmashauri imetoa shilingi milioni 275 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Itetemia ambapo ujenzi wa jengo la huduma za wagonjwa wa nje (OPD) na jengo la maabara umekamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2024/2025 Serikali imetenga shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Uyui Manispaa ya Tabora. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati katika Manispaa ya Tabora.