Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Rehema Juma Migilla
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ulyankulu
Primary Question
MHE. REHEMA J. MIGILLA K.n.y. MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuondoa upungufu wa vituo vya afya katika Kata za Tabora Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali madogo ya nyongeza. Kituo cha afya kilichopo katika Kata ya Tumbi na Misha vina upungufu mkubwa sana wa vifaatiba na watumishi. Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha inatatua tatizo hilo?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Zahanati iliyopo katika Kata ya Nhwande katika Jimbo langu la Ulyankulu, ina upungufu mkubwa wa vifaatiba na watumishi hali inayopelekea kifaatiba aina ya darubini chenye zaidi ya miaka 10, kutokuwa na mtaalamu wa ku-operate hicho kifaa. Je, nini mkakati sasa wa Serikali kuhakikisha inatupatia mtaalamu ili kuwapunguzia wananchi wangu mzigo wa kutembea umbali mrefu kupata huduma za maabara? (Makofi)
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rehema Migilla kwani amekuwa akifanya ufuatiliaji wa masuala ya maendeleo katika Jimbo lake la Ulyankulu.
 
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali lake la kwanza katika Kata ya Tumbi na Misha kwamba vituo vya afya vina uhitaji wa vifaatiba pamoja na watumishi kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya, ninaomba nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika Serikali ya Awamu ya Sita ataona kwamba bajeti kwa ajili ya vifaa na vifaatiba imeongezeka maradufu.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2020/2021 bajeti katika upande huu wa vifaa na vifaatiba ilikuwa ni shilingi bilioni 35, lakini mpaka wakati huu kila mwaka bajeti hiyo imeongezeka na sasa tuna bajeti ya shilingi bilioni 181 katika upande wa kununua vifaa na vifaatiba katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya msingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba haya ni maombi mahususi na tutayafanyia kazi kimahususi kabisa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vifaa na vifaa vifaatiba vinapatikana katika vituo vya afya hivi vya Tumbi na Misha. 
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na watumishi, Serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada ya afya kwa ajili ya kuja kutoa huduma bora kabisa za afya katika vituo vyetu hivi na kwenye upande huu, kwa sababu ajira zinaendelea katika upande huu. 
Mheshimiwa Naibu Spika, tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba katika ajira zinazokuja hizi za watumishi wa kada ya afya, tutaleta watumishi kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora za afya katika jimbo lake.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na zahanati hii ambayo na yenyewe ina uhitaji wa vifaatiba, lakini ina uhitaji wa watumishi, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutafanya hivyo kwa kuhakikisha kwamba tunafika katika zahanati hiyo kwa ajili ya kuhakikisha vifaatiba vinapatikana.
Mheshimiwa Naibu Spika, ombi hili la mtumishi na mtaalamu wa maabara, ni ombi mahususi na nitalifanyia kazi kwa umahususi wake tutawasiliana kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mtaalamu huyu anapatikana, anakuja kwenye jimbo lake kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya.
							
 
											Name
Aziza Sleyum Ally
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. REHEMA J. MIGILLA K.n.y. MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuondoa upungufu wa vituo vya afya katika Kata za Tabora Mjini?
Supplementary Question 2
MHE. AZIZA S. ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru. Kwa kuwa kuna upungufu wa vituo vya afya Mkaoni Tabora, je, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza pato katika hospitali ya mkoa kutokana na wananchi wengi wanaoenda kupata huduma katika hospitali ya mkoa? (Makofi)
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Aziza kwa swali lake zuri kabisa lenye manufaa ya kuboresha katika sekta hii ya afya. 
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa na kuimarisha sekta hii muhimu ya afya msingi. Serikali inaboresha miundombinu na inaendelea kuleta fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika sekta hii muhimu. Hata katika mwaka huu wa bajeti, tayari shilingi bilioni 53.5 zimetengwa na tayari zimeanza kutolewa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati katika kila jimbo. Serikali itaendelea na jitihada hizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na kuendelea kuongeza bajeti kwenye upande wa hospitali ya mkoa Serikali itafanya hivyo na tutawasiliana na wenzetu wa Wizara ya Afya, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaendelea kufanya uwekezaji katika sekta hii muhimu kwa maana sekta hii ndiyo inachochea maendeleo katika sekta nyingine za kiuchumi. Wananchi wetu wakiwa wana afya, wataweza kufanya kazi na nchi itapata maendeleo. Serikali itaendelea na uwekezaji kwenye sekta hii muhimu.
							
 
											Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. REHEMA J. MIGILLA K.n.y. MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kuondoa upungufu wa vituo vya afya katika Kata za Tabora Mjini?
Supplementary Question 3
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Mama Samia inasema na kutenda; na Tarime Vijijini Susuni tayari wameshaingiziwa shilingi milioni 250 kwa kituo cha afya.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu, Serikali ipo tayari kutoa maelekezo mahususi kwenye halmashauri zenye mapato makubwa kama Tarime Vijijini ili waendelee kutenga fedha kila mwaka wa bajeti ili kujenga vituo vya afya kata zote zipate vituo vya afya ili watu wapate huduma? Ahsante.
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimpongeza Mheshimiwa Waitara kwa swali lake hili zuri. 
Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhahiri kabisa kwa misingi ile ya ugatuzi wa madaraka kutoka Serikali kuu kwenda kwenye mamlaka zetu za Serikali za Mitaa; jukumu la mamlaka zetu za Serikali za Mitaa, jukumu la msingi ni kuhakikisha kwamba linapanga, linakusanya fedha na kufanya maendeleo katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi. 
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, jukumu la ujenzi na uwekezaji katika huduma za msingi ikiwemo katika sekta ya afya ni jukumu la msingi la Mamlaka zetu za Serikali za Mitaa, Serikali Kuu inakuja kuongeza nguvu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, japokuwa kuna fedha ambazo zinatoka Serikali kuu, mathalani tayari mmepokea shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuanza kujenga kituo cha afya cha kimkakati katika jimbo lako Mheshimiwa Mbunge, lakini hilo au uwekezaji huo hautoi jukumu la msingi la mamlaka ya Serikali za Mtaa kwa maana ya halmashauri kupitia mapato ya ndani kukusanya fedha na kuweka katika mipango na bajeti kwa ajili ya kuendelea kufanya uwekezaji katika upande huu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri aweze kuendelea kutimiza wajibu wa msingi kupitia mapato ya ndani watenge fedha kwa ajili ya kuendelea kujenga vituo vya kutolea huduma za msingi kabisa hizi za afya katika jimbo lako Mheshimiwa Mbunge.