Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 436 2025-05-28

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI auliza:-

Je, lini Kiwanda cha Asali cha Sao Hill kilichopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kitanunua asali kutoka kwa wananchi?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha kuchakata asali cha Sao Hill kinasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo kwa kuanzia kinatoa huduma za uchakataji wa mazao ya nyuki yanayozalishwa na TFS pamoja na wananchi kutoka vijiji jirani. Hata hivyo, kwa sasa Kiwanda hakijaanza kununua mazao ya nyuki ikiwemo asali kutoka kwa wananchi kwa kuwa mfumo wa uendeshaji wa Wakala za Serikali hautoi mwanya huo kibiashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuimarisha masoko ya bidhaa za nyuki na kujenga misingi imara ya ubora wa mazao hayo imeanzisha kampuni tanzu chini ya TFS ijulikanayo kama Misitu Company Ltd, ambayo pamoja na mambo mengine itajikita katika kununua mazao ya nyuki kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wananchi watakaohudumiwa na Kiwanda cha Asali Sao Hill.