Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI auliza:- Je, lini Kiwanda cha Asali cha Sao Hill kilichopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kitanunua asali kutoka kwa wananchi?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa wananchi wengi wa Wilaya ya Iringa Vijijini, na Kilolo pia wamehamasika sana kufuga nyuki; je, hiyo Kampuni ya Misitu Company itakuwa tayari sasa kufungua vituo katika wilaya hizo nyingine na kuwapatia elimu wananchi ili waweze kufuga nyuki katika Mkoa wetu wa Iringa? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Mkoa wetu wa Iringa maeneo ya Ikula, Mtandika Mkoa wetu wa Iringa maeneo ya Ikula, Mtandika, Msosa, Ruaha Mbuyuni, Mahenge na Nyanzwa katika Wilaya ya Kilolo wamekuwa wanavamiwa mara kwa mara na tembo. Je, Serikali ipo tayari sasa kuwapatia mizinga ya kufuga nyuki vikundi katika maeneo hayo? (Makofi)
 
											Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 20 mwezi huu, Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizindua rasmi Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Ufugaji Nyuki nchini. Kupitia Mpango huu sekta ya ufugaji nyuki inapewa kipaumbele ya kuhakikisha kwamba wananchi wanajengewa uwezo. 
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, tunaenda kuunganisha nguvu za kufungua masoko ya uuzaji wa asali na mazao yake kama ambavyo tumefungua Soko la China ambapo lina uhitaji mkubwa wa mazao ya asali. Kwa hiyo, Kampuni ile itafungua vituo kwenye maeneo mbalimbali nchini ili kuweza kununua asali za wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa kwenye maeneo yale zipo kampuni tatu binafsi zinanunua asali. Ninaomba wananchi watumie kiwanda kile kuongeza thamani ya mazao yao ili iwe rahisi kuuza mazao yao kwa kampuni hizi tatu ambazo tayari zinanunua asali kwenye eneo lile.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na ugawaji wa mizinga ya nyuki kupitia mkakati huu ambao tumeuzindua, wananchi nchi nzima watakuwa na fursa ya kuweza kupatiwa mizinga ya kufugia nyuki ili tuweze kuongeza uzalishaji kaika nchi yetu kutoka tani 34,000 za sasa tuweze kufikia tani 75,000.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved