Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 438 2025-05-28

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali kupitia TANROADS itajenga kipande cha barabara eneo la Matonga – Ifakara Mjini kama mchepuko wa barabara kubwa ya sasa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kipande cha barabara eneo la Matonga, Ifakara Mjini kwa sasa hakipo chini ya usimamizi wa TANROADS wala TARURA. Hivyo, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali itaanza taratibu za kuitambua barabara hii kwa kuifanyia tathmini na kuipanga katika daraja husika. Baada ya kuipanga katika daraja husika ambalo litaonyesha itakuwa chini ya wakala gani kati ya TANROADS na TARURA, wakala husika itaanza taratibu za kuijenga kwa kiwango cha lami, ahsante.