Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali kupitia TANROADS itajenga kipande cha barabara eneo la Matonga – Ifakara Mjini kama mchepuko wa barabara kubwa ya sasa?

Supplementary Question 1

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali kwa barabara hiyo ambayo katika halmashauri yetu, tayari tumeiita barabara ya TANROADS. Naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kuna barabara yetu ya Ifakara kwa maana ya Kikwawila, Mbasa, Lipangalala kwenda Malinyi ni lini ujenzi wake utaanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Mheshimiwa Rais alipofanya ziara, Waziri wa Ujenzi alihutubia wananchi kusisitiza juu ya ahadi yetu ya taa za barabarani katika barabara mpya ya Ifakara - Kidatu kwa maana ya taa katika Daraja la Ruaha, taa katika eneo la Muhaya Mang’ula kona na taa katika mji wa Ifakara. Je, ni lini taa hizo zitaanza kufungwa? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na swali la kwanza, lini barabara itajengwa? Tumeshasaini mkataba na mkandarasi kuanza kuijenga barabara ya Ifakara kwenda Malinyi, lakini tutaanza kwa awamu na tutaanza na kilometa 112 ambazo zitaanza Ifakara, - Lupilo hadi Mtindira kilometa 112. Kwa hiyo, tumeshasaini na tumeshaomba tayari fedha ya advance ili mkandarasi aanze kujenga na utaratibu tutakaotumia utakuwa ni Sanifu, Jenga.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu taa za barabarani, ni kweli kwamba kwa sasa kila usanifu tunavofanya ni kuweka barabara, lakini kwenye miji kuweka taa, bahati mbaya sana hiyo barabara japo imekamilika sasa hivi, lakini ilikuwa imesanifiwa miaka ya nyuma na ilianza siku kidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa miji iliyopo kama tulivyoahidi, tunamhakikishia Mheshimiwa Asenga kwamba tutaweka taa ama kwa utaratibu ambao tumeuweka wa kununua taa zote. Pia Meneja wa Mkoa wa Morogoro alishaleta mahitaji ya miji yake yote ambayo inapita hiyo barabara ili kuweza kuiwekea taa, ahsante.

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali kupitia TANROADS itajenga kipande cha barabara eneo la Matonga – Ifakara Mjini kama mchepuko wa barabara kubwa ya sasa?

Supplementary Question 2

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, Je, ni lini mkandarasi aliyepewa kazi ya kufungua barabara kutoka Kipatimu kwenda Nyamwage ataanza kazi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, mkandarasi huyo alichokuwa anasubiri ni malipo na tayari tumeshapokea maombi yake, tumeshawasilisha Wizara ya Fedha ili kazi ya kuifungua hiyo barabara ianze, ahsante.

Name

Mussa Azzan Zungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilala

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali kupitia TANROADS itajenga kipande cha barabara eneo la Matonga – Ifakara Mjini kama mchepuko wa barabara kubwa ya sasa?

Supplementary Question 3

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, barabara hii ya Jangwani kutoka Kigogo kupanda juu kwenda Klabu ya Yanga imechafuka vibaya sana. Ni barabara ambayo inaleta msongamano mkubwa sana, na pale kuna Klabu maarufu. Siyo jambo jema, na wananchi wanateseka. (Makofi)

Kwa hiyo, hebu ifanyieni kazi, matengenezo madogo tu kipande kati ya mita 20 tu pale, sawa. Toa maelekezo basi, waje wasikie watu wako.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie nafasi hii kumwelekeza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam ahakikishe kwamba leo hii anakwenda kwenye hiyo barabara na kutatua changamoto ambayo ipo ili kuondoa changamoto ambazo wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na hasa Jimbo la Ilala wanapata, ahsante. (Makofi)