Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 439 2025-05-28

Name

Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU DAU HAJI aliuliza: -

Je, lini Serikali itatengeneza barabara ya Hombolo kwa kiwango cha lami ili iweze kupitika wakati wote?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Ihumwa – Hombolo – Gawaye yenye urefu wa kilometa 55.65 kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami unaendelea na unatarajiwa kukamilika tarehe 31 Mei, 2025. Baada ya kazi hiyo kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Ahsante.