Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU DAU HAJI aliuliza: - Je, lini Serikali itatengeneza barabara ya Hombolo kwa kiwango cha lami ili iweze kupitika wakati wote?

Supplementary Question 1

MHE. MWANTUM DAU HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwanza nimshukuru Waziri wangu kwa hoja yake nzuri aliyoitoa hapo. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Je, lini kazi ya ujenzi itaanza katika barabara hiyo?

Swali langu la pili, je, Serikali ina mpango wa kumpata mkandarasi wa kusaini na kuendelea kufanya kazi hiyo?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kwa pamoja ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hii barabara ni kweli ni muhimu sana. Tumekadiria iishe tarehe 31, lakini tunavyoongea ni kwamba usanifu umeshakamilika na tulikuwa tunajua itakamilika mwaka huu wa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwanza, tumeipangia katika mwaka wa fedha unaokuja barabara hii ianze kujengwa kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, mwaka ujao wa fedha 2025/2026 tumeshaiingiza kwenye mpango ili barabara hii muhimu sana katika Mji wa Dodoma huu kwenda Hombolo ianze kujengwa kwa kiwango cha lami, ahsante.