Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 440 2025-05-28

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajengwa kwa kiwango cha lami barabara ya Njiapanda - Mang’ola – Matala hadi Lalago ambayo ipo kwenye Ilani ya CCM 2020/2025?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa Kina wa barabara ya Njiapanda - Mang’ola – Matala - Lalago yenye urefu wa kilometa 328 umekamilika. Ujenzi wa barabara hii utafanyika kwa awamu ambapo kwa sehemu ya Nkoma hadi Lalago kilometa 65 Mkandarasi yupo katika hatua za awali za kuanza ujenzi. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu iliyobaki ya Nkoma – Matala – Njiapanda ambayo itakuwa na urefu wa kilometa 263. Ahsante.