Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: - Je, lini Serikali itajengwa kwa kiwango cha lami barabara ya Njiapanda - Mang’ola – Matala hadi Lalago ambayo ipo kwenye Ilani ya CCM 2020/2025?

Supplementary Question 1

MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Naibu Spika, je, kwa kuwa barabara hii kwa upande wa Lalago Serikali imeweza kutoa kilometa 65, ni mpango upi Serikali wanao kwa upande wa Karatu kwenda Mang’ola kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara wanaopeleka mazao yao nje ya nchi kwa njia hii ya kupitia Karatu - Mang’ola?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli hii barabara ni moja, lakini tumeanza upande wa Nkoma kwenda Lalago. Kwa kuwa tumeshafanya usanifu na tumeshaitengea hata fedha katika mwaka ujao wa fedha 2025/2026, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mpango upo wa kuijenga hiyo barabara kuanzia Karatu kuelekea Matala. Ahsante.

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: - Je, lini Serikali itajengwa kwa kiwango cha lami barabara ya Njiapanda - Mang’ola – Matala hadi Lalago ambayo ipo kwenye Ilani ya CCM 2020/2025?

Supplementary Question 2

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Katika barabara iliyotajwa, ndiyo barabara ambayo ikianzia pale Njia Panda kuna Hospitali ya Wilaya takribani kilometa tatu. Kwa umuhimu wa huduma hiyo ya afya katika eneo hilo, Serikali haioni kuna haja sasa angalau hizo kilometa chache zijengwe kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue ombi la Mheshimiwa Mbunge wa hizo kilometa tatu na Wizara tuweze kuona umuhimu wa kuijenga hiyo barabara kilometa tatu kwa ajili ya kutoa huduma katika hiyo hospitali. Ahsante.

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: - Je, lini Serikali itajengwa kwa kiwango cha lami barabara ya Njiapanda - Mang’ola – Matala hadi Lalago ambayo ipo kwenye Ilani ya CCM 2020/2025?

Supplementary Question 3

MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini mwendelezo wa barabara ya Amani Makolo, Ruanda hadi Lituhi utaendelea?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, tulishaanza kujenga hiyo barabara na kipande cha Ruanda kwenda Ndumbi. Mkandarasi amesaini, lakini ambacho tunasubiri sasa hivi mkandarasi aweze kulipwa advance ili aweze kuanza kazi site.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: - Je, lini Serikali itajengwa kwa kiwango cha lami barabara ya Njiapanda - Mang’ola – Matala hadi Lalago ambayo ipo kwenye Ilani ya CCM 2020/2025?

Supplementary Question 4

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Sanzati - Nata imekuwa kero kwa muda mrefu sana na Wizara inafahamu kinachoendelea. Ni nini sasa mkakati wa Serikali wa kumaliza barabara hiyo? Nakushukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa Serikali kwa barabara zote, hasa zile ambazo wakandarasi wameshaanza, ni kuhakikisha kwamba tunazikamilisha. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mkandarasi alikuwa anasuasua kwa sababu alikuwa bado hati za malipo alizoomba zilikuwa bado hazijalipwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara ya Fedha imeahidi itatoa fedha muda siyo mrefu ili wakandarasi sasa waweze kuendelea na kazi ikiwa ni pamoja na hiyo barabara ya Sanzati - Nata.