Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 442 2025-05-28

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:-

Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha zao la Pamba na Alizeti linastawishwa kisasa ili kuinua uchumi wa Wananchi mkoani Simiyu?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali katika kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo ikiwemo pamba na alizeti. Mikakati hiyo ni pamoja na kusambaza mbegu za pamba tani 28,800, chupa 10,000 na vinyunyizi 100,000 vyenye thamani ya shilingi bilioni 50.11; kusambaza mbegu bora za alizeti tani 700 kwa wakulima kwa mpango wa ruzuku; kuajiri Maafisa Ugani 413 kupitia programu ya Jenga Kesho iliyo Bora kwa ajili ya kutoa huduma za ugani kwa wakulima; na kuwezesha utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima kwa kununua na kusambaza pikipiki 179 kwa Maafisa Ugani ngazi ya kata na vijiji na gari moja ngazi ya mkoa ili kuimarisha uratibu wa ufuatiliaji wa shughuli za ugani.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali itasambaza mbegu za pamba tani 28,000, chupa 12,000,000 na vinyunyizi 100,000 kwa wakulima wa pamba pamoja na kusambaza mbegu bora za alizeti tani 2,150 kupitia mpango wa ruzuku.