Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha zao la Pamba na Alizeti linastawishwa kisasa ili kuinua uchumi wa Wananchi mkoani Simiyu?
Supplementary Question 1
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha msimu ujao mbegu za pamba na alizeti zinafika kwa wakati katika Mkoa wa Simiyu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Je, Serikali ina mkakati gani wa dhati katika kuhakikisha kuwa zao la pamba, yaani kuhakikisha kuwa Serikali inatafuta masoko ya nje ili kuhakikisha zao la pamba bei inakuwa juu?(Makofi)
 
											Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
								NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Swali la kwanza la nyongeza la Mheshimiwa Minza kuomba mbegu za mazao haya zifike kwa wakati, hilo tunakuhakikishia kabisa mbegu zitafika kwa wakati kwenye eneo hili ili wakulima waweze kununufaika na uwepo wa mbegu katika maeneo yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kutafuta soko la pamba nje ya nchi, kama tulivyowasilisha kwenye bajeti ya Wizara hii ya Kilimo, Serikali imeweka mkakati wa kupandisha thamani ya mazao ya Tanzania katika soko la nje na Mheshimiwa Waziri alieleza kwa ufafanuzi mkubwa kabisa juu ya mshikamano kwa wakulima wa pamba katika kuhakikisha wanakidhi zile sifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, utakumbuka kuwa Mheshimiwa Waziri wa Kilimo alitoa tahadhari kwamba wakulima wa pamba wanachanganya mazao katika zao la pamba, wanaweka na mazao mengine ambayo hayana sifa ya kukaa na pamba. Kwa hiyo, tunaendelea kuimarisha kwanza wenyewe kujitafakari juu ya kilimo bora cha pamba na baadaye tulitafutie soko la nje ili wananchi waweze kuimarisha maisha ayao. 
							
 
											Name
Asha Abdullah Juma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha zao la Pamba na Alizeti linastawishwa kisasa ili kuinua uchumi wa Wananchi mkoani Simiyu?
Supplementary Question 2
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi. Je, Serikali ina mpango au mkakati gani wa kuwashawishi na kuwaelimisha wakulima wa pamba kuhusu kilimo hai (organic cotton), ambao una soko kubwa, bei ya juu, na utaleta tija zaidi kwa wakulima?
 
											Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi na mikakati ambayo Serikali tumeendelea kuwa nayo, hii hoja ya Mheshimiwa Mbunge tunaichukua kwa ajili ya kuangalia mazingira, lakini bado niendelee kusisitiza wakulima wa pamba kuzingatia yale masharti ya kilimo cha pamba ambayo tukiyazingatia yataleta tija kubwa sana kwa wakulima wetu. Ahsante sana.
 
											Name
Bupe Nelson Mwakang'ata
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha zao la Pamba na Alizeti linastawishwa kisasa ili kuinua uchumi wa Wananchi mkoani Simiyu?
Supplementary Question 3
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Mkoa wa Rukwa tunalima sana zao la miwa. Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha zao hili linastawishwa na kulimwa kisasa? Ahsante.
 
											Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
								NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Mkoa wa Rukwa, kwanza kabisa ni kuimarisha kilimo hiki cha miwa na baadaye kufikiria kuwa na kiwanda cha sukari katika eneo hili, ambapo litakwenda kuinua matarajio ya wakulima wa miwa. 
Mheshimiwa Naibu Spika, kama tulivyoeleza, tunajitahidi kuwasambaza wataalam wetu wa kilimo ili kuwasaidia wakulima. Nitoe wito tu kwa wataalamu wetu walioko Mkoa wa Rukwa kuwatembelea wakulima wa kilimo cha miwa na kufanya maboresho ili miwa yao ipate thamani inapokwenda sokoni.
							
 
											Name
Zaytun Seif Swai
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha zao la Pamba na Alizeti linastawishwa kisasa ili kuinua uchumi wa Wananchi mkoani Simiyu?
Supplementary Question 4
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha kilimo cha mbogamboga kinafanywa kisasa ili kuwainua kiuchumi wananchi wa Wilaya za Meru na Arumeru?
 
											Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo cha mbogamboga ni kilimo cha kimazingira vilevile, yaani siyo kila mahali patastawi mboga hizi za bustani, lakini mkakati wa Serikali katika kuimarisha kilimo hiki. Tumeanza kusambaza watalaam kwenda kwenye maeneo mbalimbali na kutoa elimu ya kutosha ili wananchi wajue namna ya kusimamia bustani zao katika kupata matokeo.
 
											Name
Shally Josepha Raymond
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha zao la Pamba na Alizeti linastawishwa kisasa ili kuinua uchumi wa Wananchi mkoani Simiyu?
Supplementary Question 5
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kutokana na jibu la msingi kwamba mbegu za alizeti zitatawanywa, tambarare ya Kilimanjaro mbegu hizo zinastawi vizuri sana. Je, wananchi wa Rundugai, Ruvu, TPC na Rombo watafikiwa na mbegu hizo?
 
											Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
								NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y WAZIRI WA KILIMO:  Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyo mkakati wa Serikali katika kuimarisha huduma hii ya utoaji wa mbegu, tunalichukua ombi la Mheshimiwa Raymond ili kuangalia maeneo hayo. Pia tuwaelekeze Maafisa Ugani wetu walioko kwenye maeneo husika, kuyapitia na kuona kama tunaweza tukawapelekea mbegu. 
Mheshimiwa Naibu Spika, mbegu zipo za kutosha, na kila mwananchi anaweza kufikiwa kulingana na vile vigezo na sifa za maeneo wanayolima zao hili.