Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 443 2025-05-28

Name

Nashon William Bidyanguze

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika Mbuga ya Kalola, Kijiji cha Nguruka – Uvinza?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa skimu za umwagiliaji za Mgambazi (hekta 1,000), Kashagulu (hekta 1,200), Nkonkwa (hekta 1,000) na Ilagala (10,000) katika Wilaya ya Uvinza kwa ajili ya kujua gharama halisi za ukarabati wa skimu hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, usanifu unaendelea katika Skimu ya Mbuga ya Kalola yenye ukubwa wa hekta 20,000 iliyopo katika Kijiji cha Nguruka kwa ajili ya kujua gharama halisi za ujenzi. Aidha, Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika mwaka 2025/2026 itakamilisha usanifu wa skimu hizo na kuanza taratibu za manunuzi ili kuwapata wakandarasi kwa ajili ya ujenzi na ukarabati.