Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Nashon William Bidyanguze

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika Mbuga ya Kalola, Kijiji cha Nguruka – Uvinza?

Supplementary Question 1

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza ni hizi Skimu za Kashagulu, Mgambazi, Nkonkwa na Ilagala, baadhi yake ziliwahi kuwa zinafanya kazi; na kwa kuwa tegemeo la wananchi ni kwenye kilimo cha umwagiliaji, je, ni lini sasa upembuzi yakinifu huu wa ukarabati utakamilika?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kwenye Skimu hii ya Kalola; hili ni bonde kubwa sana kama Serikali inavyotambua kwamba ni hekta 20,000. Hii skimu ikienda kujengwa itahudumia na kufaidisha wananchi takribani 100,000. Je, ni lini hii skimu pia itakwenda kukamilika upembuzi yakinifu wake? Ahsante. (Makofi)

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, tayari shughuli ya upembuzi yakinifu na upembuzi wa kina zinaendelea katika maeneo yote haya niliyoyataja ikiwemo hii skimu ya Kalola. Serikali inajua kabisa na kutambua umuhimu wa skimu hizi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kweli kwa kufuatilia jambo hili, na nikuhakikishie katika mwaka ujao wa fedha 2025/2026 tayari mmeshatupitishia bajeti ya kwenda kutekeleza jukumu hili, ninawaomba wananchi wa maeneo haya yote wawe watulivu wakati Serikali inaendelea kutekeleza ukamilishaji wa skimu hizi.

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika Mbuga ya Kalola, Kijiji cha Nguruka – Uvinza?

Supplementary Question 2

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante nikushukuru kwa nafasi. Skimu ya Umwagiliaji katika mtaa wa Gendi Kuu, Kata ya Singe, Jimbo la Babati Mjini ulitakiwa kuanza baada ya mvua kukatika na mvua zimeshakatika, hazinyeshi tena. Ni lini skimu hii itaanza, kwani wananchi wanasubiri?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tumpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji. Kama alivyojieleza yeye mwenyewe, ni kweli kabisa mvua zimepungua. Ninaelekeza watalaam wetu waende site kule kuangalia uwezekano wa kuanza kwa skimu hii, ahsante.