Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Water and Irrigation Wizara ya Maji 444 2025-05-28

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza inapatikana katika maeneo yote nchini ikiwemo maeneo ya Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria. Katika kutimiza azma hiyo, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa miradi ya maji itakayonufaisha Kata hizo tano zilizopo ndani ya Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 itakarabati Skimu za Iroba, Kinagi, Goziba na Ikuza zilizopo katika Kata hizo ili ziendelee kutoa huduma ya maji kwa wananchi kwa ufanisi wakati taratibu za kutekeleza miradi mipya zikiendelea.