Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Supplementary Question 1

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kisiwa cha Goziba ambacho mara nyingi hupata milipuko ya magonjwa yatokanayo na ukosefu wa majisafi na salama, water pump yake haifanyi kazi. Kwa nini RUWASA Mkoa wa Kagera wasiweze kuingilia kati waweze kutengeneza hizi water pump ili wananchi waweze kupata maji? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili wananchi wa Kerebe kupitia Mbunge wao wa Jimbo Mheshimiwa Mwijage, walishanunua water pump inayotumia diesel. Kwa nini RUWASA, Mkoa wa Kagera wasijenge mtandano wa maji ambao utawasaidia wananchi hawa ili kuwatua ndoo akina mama? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge, dada yangu Oliver amekuwa akifuatilia sana katika suala hili la eneo la Goziba.

Mheshimiwa Naibu Spika, pump iliyoharibika iliharibika na huu mradi ulikuwa ukiendeshwa na Halmashauri, lakini kwa sasa hivi Wizara imeingilia kati. Nimpongeze sana Mheshimiwa Aweso, ameshatoa maelekezo kwa Regional Manager wa Kagera ili aweze kufika hapo kuhakikisha hii water pump inafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika Kisiwa cha Kerebe kwa Kaka yangu Mheshimiwa Mwijage ninamtoa hofu Mheshimiwa Oliver pamoja na kaka zake wote ambao anaendelea kushirikiana nao, Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo, ule mtandao wa maji nao unaenda kufanyiwa tathmini ili wananchi wale waweze kupatiwa maji. Maagizo haya tayari Mheshimiwa Waziri Aweso ameshamwagiza RM - Kagera.

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Supplementary Question 2

MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata ya Old Moshi Mashariki yenye vijiji vinne vya Kidia, Tsuduni, Mahoma na Kirara, Kata hii haijawahi kupata maji kabisa, lakini kuna miundombinu ya mabomba ambayo wamelaza chini na hawajaweza kuwapelekea maji.

Je, Serikali haioni haja ya kupeleka maji katika Kata hii ili kuepusha wananchi na magonjwa ya mlipuko? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpongeze pia Mheshimiwa Felister Njau kwa swali zuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, mabomba yamepita, sasa ni utekelezaji. Tayari kama unavyoona miradi mingi imekamilika na maji ni mwa mwa mwaaa, kwa hiyo, nimatoe hofu, vijiji hivi vinne vya Old Moshi nao watakwenda kunufaika na huduma hii ya kumtua Mama ndoo kichwani na Mheshimiwa Aweso ameniagiza niseme, wote ambao mnafuatilia masuala haya ya miradi ya maji yanakwenda kukamilika. (Makofi)

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Supplementary Question 3

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Nianze kwa kuishukuru Serikali kwa sababu imetoa zaidi ya shilingi milioni 800 kufanya ukarabati wa miundombinu ya maji katika Kata ya Old Moshi Mashariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tumeshaiomba Serikali ilete fedha kumalizia usambazaji wa mabomba katika Kata hii, na katika bajeti ya mwaka huu nimepewa fedha, kwa hiyo, tusipotoshe watu hapa. Serikali inafanya kazi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba unilinde. Serikali inafanya kazi na imetoa fedha za kufanya ukarabati wa miundombinu ya maji katika Kata hii. Nashukuru. (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakupongeza sana Baba yangu, Mheshimiwa Prof. Ndakidemi kwa kazi nzuri anayoifanya. Ninamshukuru pia kwa moyo wa shukrani, kwa sababu wanasema moyo usiokuwa na shukrani hukausha mema yote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hizi shilingi milioni 800 ambazo Wizara ya Maji imeshazielekeza katika eneo hili la Old Moshi, nikutoe hofu, Serikali itakuja kukamilisha hizi fedha na huu mradi utakamilika kwa kuhakikisha usambazaji unafikia maeneo yote yalivyotakiwa kufikiwa. (Makofi)

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Supplementary Question 4

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Wananchi wangu wa Kata ya Nyakatuntu wanatembea umbali mrefu kwenda kwenye chanzo cha maji kinachoitwa Kitoboka, ni mbali sana. Ninataka kujua, ni lini hawa wananchi watapatiwa majisafi ya bomba kwenye maeneo yao?(Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge. Eneo la Nyakatuntu katika mwaka ujao wa fedha nao wataingia katika usanifu na kuhakikishiwa wanafikiwa na huduma ya majisafi na salama. (Makofi)

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Supplementary Question 5

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa maji wa kutoka Hatete kwenda Ihowa, Rumbila, Weru hadi Myovizi, ni lini mradi utaanza kujengwa?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninampongeza Mheshimiwa Hasunga kwa ufuatiliaji mzuri. Maeneo haya yote aliyoyataja Ihowa pamoja na kule kwingine, kadri fedha inavyopatikana Wizara ya Maji itahakikisha mradi huu unakuja kujengwa ndani ya muda. (Makofi)

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Supplementary Question 6

MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na changamoto kubwa ya maji katika Kata ya Nguruguru iliyoko ndani ya Wilaya ya Ileje. Je, ni upi mpango wa Serikali kuhakikisha wananchi hawa wanapata majisafi na salama ili kuepusha changamoto za kiafya kwa wananchi hawa? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji mzuri sana. Kata hii ya Nguruguru pale Ileje, mpango wa Serikali ni kuhakikisha maeneo yote haya yanafikiwa na huduma ya majisafi na salama. Kadri fedha inavyopatikana, tutahakikisha miradi inapelekwa kule na usambazaji pia unawafikia wananchi wote. (Makofi)

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Supplementary Question 7

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tenki la kukusanyia maji kutoka Lake Victoria, tayari limeshajengwa Wilayani Urambo eneo la Muungano. Je ni lini Serikali itaanza kuweka usambazaji wa mabomba kuelekea kule ambako maji yanatakiwa kufika? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, tenki tayari. Kwanza tumpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa namna ambavyo amehakikisha mradi huu wa Miji 28 Urambo nao wananufaika. Usambazaji wa mabomba nikutoe hofu Mheshimiwa Sitta, kadri fedha zinavyopatikana, kadri muda unavyoendelea ataona kazi ikikamilika kwa sababu kazi kubwa tayari imeshafanyika. (Makofi)

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Supplementary Question 8

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata za Kwekivu na Masagalu zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji na hata yakichimbwa muda mwingine hayapatikani maji baridi, yanakuwa ni chumvi iliyopitiliza. Je, ni upi mkakati wa Serikali kupeleka maji katika Kata hizi mbili? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninampongeza sana Mheshimiwa Husna Sekiboko kwa ufuatiliaji mzuri. Kama anakumbuka, nilipokuwa Wizara ya Maji nilifika kule, naye mwenyewe alishuhudia kazi nzuri iliyokuwa ikifanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimtoe hofu kwamba wataalam wetu wanaendelea kuchakata namna njema ya kuhakikisha wananchi hawa wa Kata hizo alizozitaja kule Kilindi na wenyewe wanaweza kupatiwa majisafi na salama. (Makofi)

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kuzipatia maji Kata za Ikuza, Mazinga, Kerebe, Goziba na Bumbire zilizopo Ziwa Victoria?

Supplementary Question 9

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kata ya Buganguzi yenye vijiji vinne, tuna mradi mkubwa wa zaidi ya shilingi bilioni tatu, mradi umejengwa zaidi ya 98%, lakini wananchi hawapati maji. Je, ni kitu gani kimekwamisha wananchi wasipate maji katika Kata ya Buganguzi?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, three billion zimeweza kutekeleza mradi huu. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Aweso, ninamwagiza Regional Manager wa Kagera, aende akakague mradi huu na ahakikishe wananchi wanapata manufaa ya fedha ambayo imeshatumika.(Makofi)