Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 34 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 445 2025-05-28

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Primary Question

MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza:-

Je, Serikali imefikia hatua gani katika jitihada zake za kuwekeza mtaji katika Kiwanda cha Kahawa cha TANICA - Bukoba Mjini?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, Kiwanda cha Kahawa cha TANICA kinamilikiwa na Kagera Cooperative Union - KCU kwa 53.37%, Karagwe District Cooperative Union - KDCU kwa 31.83%, Msajili wa Hazina 7.67%, Tanzania Federation of Cooperative - TFC 6.22% na Wafanyakazi wa TANICA 0.91%.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilifanya tathmini ya kiwanda hicho na kubaini kuwa kiwanda hakikuwa na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti nzuri. Serikali imesimamia kuundwa kwa Bodi ya Wakurugenzi na kwa sasa kiwanda kinaendelea kufanyia kazi ushauri mbalimbali unaotolewa na Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kushirikiana na wanahisa wakuu wa kiwanda ili kumtafuta mwekezaji mahiri atakayeingiza mtaji kwenye Kampuni ya TANICA. Ninakushukuru sana.