Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 13 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 156 2026-04-21

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: -

Je, kwa nini Mahindi yanayovunwa kutokana na Mbegu za kisasa hayawezi kupandwa kwa mara ya pili?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mkulima hulazimika kununua mbegu kila msimu ili aweze kupata tija iliyodhamiriwa kwa sababu mbegu anazonunua katika maduka ya pembejeo huwa zimepitia majaribio ya kisayansi katika maabara ili kuthibitisha ubora wa sifa mbalimbali ikiwemo kiwango cha uzalishaji, uhimilivu wa magonjwa na ukame. Mkulima anapovuna mazao na kutumia mbegu kwa mara ya pili au zaidi husababisha sifa stahiki za mbegu husika kupungua au kupotea.

Mheshimiwa Spika, asilimia kubwa ya mbegu zinazotumiwa na wakulima nchini ni mbegu aina ya chotara ambazo utengenezaji wake hutumia aina mbili au zaidi tofauti za mbegu wazazi kutoka jamii moja. Kutokana na sababu hiyo, iwapo mbegu hizo zitatumika kama mbegu kwa mara ya pili au zaidi husababisha kupotea au kupungua kwa ubora wa mbegu hizo na hivyo kuchangia kushuka kwa tija na uzalishaji.