Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 22 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 248 2026-05-05

Name

Cornel Lucas Magembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato Kaskazini

Primary Question

MHE. CORNEL L. MAGEMBE aliuliza: -

Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Nyamirembe, Nyabugere, Katende na Magiri ambazo zimechakaa sana?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Cornel Lucas Magembe, Mbunge wa Jimbo la Chato Kaskazini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu chakavu au ujenzi wa miundombinu mipya katika shule ambazo miundombinu yake haiwezi kukarabatiwa. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2025/2026 Serikali imetoa shilingi bilioni 3.09 kwa ajili ya ujenzi shule za msingi 11, madarasa 153 katika shule chakavu 24 na ukamilishaji wa madarasa matatu katika Shule za Msingi Nyamirembe na Magiri Wilayani Chato.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imetenga shilingi 150,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa sita katika Shule za Msingi Katende na Nyarubugere. Aidha, Serikali itaendelea kutenga fedha za ukarabati au ujenzi wa miundombinu mipya katika shule za msingi chakavu nchini ikiwemo Shule za Msingi Nyamirembe, Nyabugere, Katende na Magiri, ahsante.