Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cornel Lucas Magembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato Kaskazini

Primary Question

MHE. CORNEL L. MAGEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Nyamirembe, Nyabugere, Katende na Magiri ambazo zimechakaa sana?

Supplementary Question 1

MHE. CORNEL L. MAGEMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Serikali imekuwa ikitenga fedha kupeleka kwenye Halmashauri ya Chato kwa ajili ya ukarabati wa shule mbalimbali za msingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye shule hizi ambazo nimemuuliza Naibu Waziri, hasa Shule ya Nyamirembe, Shule ya Nyabugera, Shule Magiri na Shule ya Msingi Katende na Shule ya Msingi Rutunguru, ni shule ambazo kwa sasa ukifika ni hatari sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, shule hizi zina zaidi ya watoto 2,000 kwa kila shule, lakini unakuta kuna madarasa matatu ambayo yanafanya kazi na madarasa mengine ni chakavu kabisa. Je, Serikali ina mpango gani wa kutumia njia za haraka ili kuhakikisha kwamba watoto hawa wanawanusuru hali hiyo? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, ni kweli kwamba shule hizi ambazo Mheshimiwa Mbunge wa Chato Kaskazini amezitaja ni shule kongwe na chakavu na ndio maana Serikali imeendelea kupeleka fedha kwa awamu kuhakikisha kwamba shule hizi ninakarabatiwa na katika kipindi cha miaka minne iliyopita Serikali imepeleka zaidi ya shilingi bilioni tatu na milioni tisini kwa ajili ya ukarabati wa shule hizi chakavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2026/2027 mwaka ujao Serikali imetenga shilingi 150,000,000 kwa ajili ya shule hizi ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja ili zikarabatiwe na ziwe na viwango vizuri kwa ajili ya kutoa huduma ya elimu kwa wanafunzi. Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Magembe, kwamba Serikali inatambua changamoto ya uchakavu wa shule zetu na ndio maana tumeendelea kutenga fedha kwa awamu na fedha hizo zitapelekwa mwaka ujao wa fedha ili kukarabati shule hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haijaishia hapo, Serikali imefanya tathmini ya uchakavu wa shule za msingi kote nchini na kutambua jumla ya shule 10,595 kongwe na chakavu ambayo tathmini ya awali inaonesha tunahitaji takribani shilingi trilioni 2.8 kwa ajili ya ukarabati. Kwa hiyo, Serikali inaendelea kuandaa mipango ya ukarabati wa shule hizo kwa awamu ili ziwe na ubora unaotakiwa kwa ajili kutoa huduma hapo shuleni. Ahsante. (Makofi)

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CORNEL L. MAGEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Nyamirembe, Nyabugere, Katende na Magiri ambazo zimechakaa sana?

Supplementary Question 2

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, miongoni mwa maeneo ambayo kuna shule chakavu sana ni pamoja na jimboni kwangu Bunda Mjini, Kata ya Wariku, shule hizo ni Kiwasi, Kangetutya na Kamkenga ni chakavu sana. Ni lini Serikali itatukarabatia ili watoto wetu wasome kwenye mazingira rafiki?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, shule hizi ambazo Mheshimiwa Mbunge wa Bunda Mjini amezitaja ni miongoni mwa shule 10,595 ambazo tulizifanyia tathmini na Serikali inaandaa utaratibu kwa ajili ya kwenda kuzifanyia ukarabati mkubwa. (Makofi)

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CORNEL L. MAGEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Nyamirembe, Nyabugere, Katende na Magiri ambazo zimechakaa sana?

Supplementary Question 3

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Shule ya Msingi Nangwa ni shule kongwe na ina zaidi ya watoto 1,000. Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati wa shule hii pamoja na shule nyingine ambazo ziko katika Jimbo la Hanang? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Shule ya Msingi Nangwa katika Jimbo la Hanang ni moja ya shule ambazo Mheshimiwa Asia Halamga ameziwasilisha kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Hanang kwamba zinahitaji ukarabati mkubwa na Serikali inatambua kwamba shule ile ina wanafunzi wengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, tumekubaliana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hanang kuanza kutenga fedha kwa awamu mapato ya ndani kufanya ukarabati mdogo mdogo ili kuwezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri wakati Serikali inaendelea na utaratibu wake wa ukarabati wa zile shule 10,595. (Makofi)

Name

Thomas Maganga Kampala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Primary Question

MHE. CORNEL L. MAGEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Nyamirembe, Nyabugere, Katende na Magiri ambazo zimechakaa sana?

Supplementary Question 4

MHE. THOMAS K. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, niipongeze Serikali kwa kuja na mkakati wa kuzitambua shule zote kongwe na chakavu. Swali langu; je, ni lini mpango huo utakamilika kwa sababu shule nyingi ikiwemo Shule ya Msingi Masigo zina hali mbaya sana? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya tathmini tayari ya idadi ya shule ambazo ni chakavu na hivi sasa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tumeshawasilisha andiko na mapendekezo kwa Wizara ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ili tufanye tathmini na kuona uwezekano wa wa kupata vyanzo vya mapato kwa ajili ya kuanza kupata fedha hizo na kuanza ukarabati wa shule hizo 10,595 kwa awamu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari Serikali imeshachukua hatua tunaendelea na taratibu na mara taratibu zitakapokamilika tutaanza ukarabati wa shule hizo katika maeneo mbalimbali kote nchini.