Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 22 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 249 2026-05-05

Name

Kiswaga Boniventura Destery

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Magu

Primary Question

MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga barabara za Mitaa Miji ya Kisesa na Bujora kwa kuwa ni miji ya kibiashara?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Jimbo la Magu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali ilitenga shilingi milioni 252.88 za matengenezo ya Barabara za Kisesa – Machinjioni na Shilabela – Kisesa kwenye Mji wa Kisesa ambapo matengenezo hayo yanaendelea kufanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imefanya usanifu wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa Barabara ya Msikitini - Mnarani kilometa 1.2 katika Mji wa Bujora ambapo makadirio ya ujenzi yatagharimu shilingi bilioni 1.5.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imeweka katika mipango yake ya bajeti kiasi cha shilingi milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa mitaro yenye urefu wa mita 3,000 kwenye barabara za Mji wa Kisesa ambazo ni Barabara ya Ngomeni, Barabara ya Kanyama - Busekwa na Barabara za Kisesa – Machinjioni.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara katika Miji ya Kisesa na Bujora ambayo ni muhimu kibiashara, ahsante.