Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Kiswaga Boniventura Destery
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Magu
Primary Question
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga barabara za Mitaa Miji ya Kisesa na Bujora kwa kuwa ni miji ya kibiashara?
Supplementary Question 1
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu ya Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Kwa Mkapa -Machinjioni ambayo inaendelea kujengwa sasa hivi inajengwa mitaro sehemu korofi peke yake. Kuna baadhi ya maeneo ambayo kwa sasa wananchi hawawezi kupita.
Je, Serikali inaweza kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha barabara hiyo kujenga mitaro ili zitosheleze kwenda mpaka mwisho wake? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kwa kuwa Serikali ilituahidi na ikaleta barua na mkataba ukaandaliwa katika Barabara ya Msikitini kwenda Minara na Ngomeni kujenga kwa kiwango cha lami, niishukuru imetenga shilingi milioni 600. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuleta fedha kwa haraka ili kukamilisha hizo barabara? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwanza, nimhakikishie Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Jimbo la Magu kwamba Serikali imekuwa ikipeleka fedha katika barabara hizi kwa awamu kuhakikisha kwamba zinajengwa kwa kiwango cha changarawe na kiwango cha lami na ndiy o maana katika bajeti ya mwaka huu tumetenga shilingi milioni 600 kwa ajili ya barabara hizo za Msikitini - Ngomeni kuhakikisha kwamba zinajengwa na zinapitika vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu tuna barabara ambayo imejengwa mitaro kwa sehemu na tunaendelea na ujenzi wa mitaro katika barabara hizo. Utaratibu wa Serikali ni kwamba yako maeneo ambayo ni hatarishi na ni rahisi kuharibika zaidi hasa wakati wa mvua. Kwa hiyo, mara nyingi tunajenga maeneo yale korofi kuweka mifereji, kuweka makaravati na madaraja na baada ya hapo tunaendelea na maeneo mengine. Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Kiswaga kwamba barabara hizo na hiyo mifereji itakwenda kujengwa. (Makofi)
Name
Mariam Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga barabara za Mitaa Miji ya Kisesa na Bujora kwa kuwa ni miji ya kibiashara?
Supplementary Question 2
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa katika Jimbo la Temeke Kata ya Tandika, Kata ya Temeke na Kata ya Azimio ni kata ambazo ziko sasa katikati ya mji. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuboresha barabara za mitaani? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Mheshimiwa mama yangu, Mheshimiwa Mariam Kisangi, Mbunge wa Temeke amekwisha wasilisha kupitia Meneja wake wa TARURA Wilaya ya Temeke orodha ya barabara hizo katika Kata ya Tandika, Temeke, Azimio na tayari Serikali imeingiza kwenye Mpango wa Bajeti wamwaka 2026/2027, yako maeneo ya barabara za mitaa ambazo zitajengwa kupitia bajeti ya kawaida ya TARURA, lakini yapo maeneo tutajenga kupitia mradi wa DMDP II.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa mama, Mheshimiwa Mariam Kisangi, kwamba, Serikali hii iko kazini na tutahakikisha barabara hizo zinaendelea kujengwa kwa awamu ili kurahisisha usafiri kwa wananchi.
Name
Sara Msafiri Ally
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga barabara za Mitaa Miji ya Kisesa na Bujora kwa kuwa ni miji ya kibiashara?
Supplementary Question 3
MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara nyingi zimekuwa zikiharibika kwenye Jimbo la Mvomero hasa maeneo wanayofanya shughuli za uchimbaji wa madini; kama Kata ya Mvomero, Kata ya Lubungo na maeneo mengine.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza bajeti kwenye maeneo hayo ya barabara ili ziweze kupitika kipindi chote cha shughuli za wananchi wanapofanya shughuli zao? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 mpaka sasa imeongeza bajeti ya TARURA kwa zaidi ya takribani mara nne na dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba barabara zetu zote za vijijini na mijini zinapitika ili kuwawezesha wananchi kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa ufanisi mkubwa zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa Sara Msafiri, Mbunge wa Jimbo la Mvomero, kwamba Serikali inatambua changamoto na hususani ya Mvomero kwa hali ya hewa mvua nyingi mafuriko na shughuli nyingine za kiuchumi ambazo zinapelekea barabara nyingi kuharibika na majimbo mengine yenye sura ya aina ya Mvomero, Serikali imeweka mpango madhubuti kuhakikisha kwamba barabara hizo zinajengwa na kupitika vizuri. (Makofi)
Name
Emanuel Qambaji Nuwas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga barabara za Mitaa Miji ya Kisesa na Bujora kwa kuwa ni miji ya kibiashara?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. EMANUEL Q. NUWAS: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kupata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa katika Jimbo la Mbulu Vijijini, kuna miji miwili mikubwa ya kibiashara na kiutawala Dongobesh na Haydom na haina barabara za kutosha. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara za mitaa kuendeleza shughuli za biashara? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Mbulu Vijijini kwa Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Dkt. Nuwas, ni kweli kwamba kuna miji ya kibiashara ikiwemo Dongobesh na Haydom na Serikali imeendelea kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za vijijini na mijini, lakini tunatambua kwamba bado kuna uhitaji wa barabara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwanza Serikali imeendelea kutanua wigo wa mtandao wa barabara za TARURA kila mwaka, na suala hilo tumewaelekeza Mameneja wa TARURA kote nchini kwa maeneo ambayo yanahitaji kuongeza mtandao wa barabara ambao ni muhimu kwa hudumu za wananchi, waendelee kuwasilisha mapendekezo ili Serikali iweze kuanza kuingiza kwenye bajeti.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pili, barabara ambazo zipo tayari Serikali imeendelea kutenga fedha na katika bajeti ya mwaka 2026/2027 Serikali imetenga fedha, lakini zile ambazo zimeathirika na mvua ambazo zinaendelea Serikali inaendelea kuuandaa utaratibu kwa ajili ya kwenda kufanya matengenezo ya dharura. (Makofi)
Name
Amosy William Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Primary Question
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga barabara za Mitaa Miji ya Kisesa na Bujora kwa kuwa ni miji ya kibiashara?
Supplementary Question 5
MHE. ENG. AMOSY W. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Mji Mdogo wa Kituo ulio Kata ya Kituo, Wilaya ya Sikonge, baadhi ya barabara zake ziko katika mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami pamoja na kufungiwa taa. Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa ujenzi wa hizo barabara? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimthibitishie Mheshimiwa Engineer Maganga, Mbunge wa Sikonge, kwamba tunafahamu kuna uhitaji wa barabara za changarawe na za lami katika miji na vijiji katika Jimbo la Sikonge na ndiyo maana kwanza tumeshapokea orodha ya mapendekezo ya barabara za kufungua, kujenga na kukarabati, lakini pia tunaendelea kuandaa bajeti na utaratibu wa kuanza kujenga barabara hizo kwa awamu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Sikonge kwamba Serikali hii sikivu itakwenda kufanya kazi hiyo kwa awamu kuhakikisha kwamba miundombinu inapitika vizuri.
Name
Juma Ramadhani Mustafa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igalula
Primary Question
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga barabara za Mitaa Miji ya Kisesa na Bujora kwa kuwa ni miji ya kibiashara?
Supplementary Question 6
MHE. JUMA M. KAWAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatana na umuhimu wa barabara ya kutoka Misole – Miyenze - Nyahua katika Jimbo la Igalula, je, ni lini Serikali italeta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kutumia nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Kawamba, Mbunge wa Jimbo la Igalula kwamba tunafahamu kwamba barabara hii ya Misole, Miyenze na Nyahua katika Jimbo la Igalula ni moja ya barabara muhimu sana katika jimbo lake na tayari imewasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI na yeye ameisemea mara kadhaa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kumhakikishia kwamba Serikali iko kwenye taratibu za kuweka mpango wa bajeti kwa ajili ya kuanza kutangaza barabara hizi na kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hizi.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga barabara za Mitaa Miji ya Kisesa na Bujora kwa kuwa ni miji ya kibiashara?
Supplementary Question 7
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru, wakandarasi wengi wa Jimbo la Bunda kwenye Barabara za Bukama, Mhingo, Nyaburundu, Kurusanga na maeneo mengine wote wametoka site wanasema hawajalipwa fedha zao za utangulizi. Ni lini sasa mtawalipa wakandarasi wa Jimbo la Bunda ili waendelee na kazi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikiwalipa wakandarasi kwa awamu na tumeanza batch ya kwanza, batch ya pili na tunaendelea kwa utaratibu huo. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Getere kwamba tutakwenda kuwalipa pia wakandarasi hao ili kuhakikisha kwamba kazi ambazo wameshapewa wanaenda kuzifanya na kuzikamilisha.