Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 22 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 251 2026-05-05

Name

Japhael Masanja Lufungija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga maghala ya kuhifadhia mazao Kata ya Uyowa katika kitovu cha biashara Mwamnange ambapo tayari eneo lipo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Wizara imepanga kufanya tathmini ya maeneo mapya ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa ghala. Tathmini hiyo itasaidia kubaini mahitaji ya uwezo wa kuhifadhi mazao katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo kuiwezesha Serikali kutenga bajeti ya kuanza utekelezaji wa ujenzi wa ghala.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kumhakikishia Mheshimiwa Japhael Masanja Lufungija kuwa suala lake limechukuliwa na litafanyiwa kazi na Serikali baada ya kufanya tathmini kwenye kata ya Uyowa katika center ya kibiashara Mwamnange.