Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Japhael Masanja Lufungija
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ulyankulu
Primary Question
MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga maghala ya kuhifadhia mazao Kata ya Uyowa katika kitovu cha biashara Mwamnange ambapo tayari eneo lipo?
Supplementary Question 1
MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Mimi nitakuwa na swali moja tu la nyongeza pamoja na majibu mazuri ya Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahadi ya ujenzi wa ghala katika senta ya Mwamnange kwenye kata ya Uyowa iliahidiwa mwaka 2023/2024, lakini majibu ya Serikali wameeleza kwamba wako tayari kufanyia kazi jambo hilo.
Je, Naibu Waziri uko tayari kuongozana na mimi baada ya Bunge hili kwenda kufanya mkutano na Wananchi wa Mwamnange ili kuhakikisha jambo hili litatekelezwa? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, ninamhakikishia tena Mheshimiwa Mbunge Japhael Masanja Lufungija kwamba niko tayari na Serikali itatekeleza ujenzi katika eneo lake. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Johannes Lembulung’ Lukumay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga maghala ya kuhifadhia mazao Kata ya Uyowa katika kitovu cha biashara Mwamnange ambapo tayari eneo lipo?
Supplementary Question 2
MHE. JOHANNES L. LUKUMAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kuniruhusu kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Arumeru Magharibi lina wakulima wazuri sana wa mazao ya mboga mboga. Wakulima hawa wanapoteza mazao yao ya mboga mboga baada ya kuvuna.
Je, Serikali itasaidia ujenzi wa vyumba vya kutunza baridi yaani cold rooms Kata ya Bangata na Kata ya Ilkiding’a ili wakulima hawa wasiendelee kupata hasara?
Mheshimiwa Naibu Spika, la nyongeza kidogo, ningemwomba Naibu Waziri kama atakubaliana na mimi kuongozana kwenda Jimbo la Arumeru Magharibi akashuhudie hao wakulima wazuri wanavyopoteza mazao yao ya mboga mboga. Ahsante sana.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, nimthibitishie tu Mheshimiwa Dkt. Johannes, Mbunge wa Arumeru Magharibi kwamba moja, niko tayari tutaongozana mara baada ya Bunge la bajeti nitafika maeneo mengi nchini, lakini la pili ni kwamba Serikali moja ya mpango tulionao ya kupunguza hii post-harvest loss ni kujenga cold rooms katika maeneo yote yanayofanya kilimo cha mboga mboga.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo lipo katika mipango ya Serikali, kwa hiyo, nitakuja kujionea na baada ya hapo tutafanya maamuzi. Ahsante sana.
Name
Prof. Pius Zebhe Yanda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buhigwe
Primary Question
MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga maghala ya kuhifadhia mazao Kata ya Uyowa katika kitovu cha biashara Mwamnange ambapo tayari eneo lipo?
Supplementary Question 3
MHE. PIUS Z. YANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na mimi ninaomba niulize swali la nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iliahidi ujenzi wa ghala la kuhifadhia tangawizi katika Kata ya Munzeze, Jimbo la Buhigwe pamoja na mitambo ya kukausha tangawizi ili kuweza kuongeza ubora wa zao hilo. Pia Serikali iliagiza halmashauri iweze kuandaa eneo la kuwekeza kuweka hilo ghala pamoja na miundombinu mingine na halmashauri ilishaandaa eneo takribani eka 15 na ikaandaa hati pacha kati ya Wizara ya Kilimo na Halmashauri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, swali langu ni kwamba, ni lini Wizara itaweza kuwezesha hilo ili wananchi waweze kunufaika na huduma hizo na kuweza kuboresha zao na tangawizi katika Wilaya ya Buhigwe?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Ninamshukuru pia Mheshimiwa Pius Yanda, Mbunge wa Jimbo la Buhigwe. Jambo moja tu nimwambie kwamba haya yote aliyoyazungumza ni sehemu ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais hususan wakati anagombea Urais katika jimbo lake la kuhakikisha tunajenga ghala katika eneo lake aliloliainisha hapo pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kukaushia tangawizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Wizara ya Kilimo tukishirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara tupo katika mpango huo wa utekelezaji na tuko katika hatua za tathmini na tukishamaliza tutafika katika eneo lake na kuanza hii shughuli. Ahsante sana.
Name
Edefonce Joackim Canoni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga maghala ya kuhifadhia mazao Kata ya Uyowa katika kitovu cha biashara Mwamnange ambapo tayari eneo lipo?
Supplementary Question 4
MHE. EDIFONSI J. KANONI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Kalambo katika Kata za Ulumi, Mnamba, Mambwe Nkoswe na Mambwekenya ni wazalishaji wakubwa sana wa mazao. Je, ni lini mpango wa Serikali kujenga maghala katika eneo hilo ili wananchi hawa wanapovuna wawe na sehemu ya kuhifadhi wakati wanasubiri soko? Ahsante sana. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na ninaomba tu nijibu kwa ujumla kama nilivyojibu katika maswali ya msingi. Moja ya jukumu kubwa tunalolifanya sasa ni kwamba imeundwa timu ya wataalam kupita na kufanya tathmini katika maeneo yote nchini ikiwemo katika jimbo lako Mheshimiwa Mbunge na baada ya kumaliza ile tathmini jukumu letu litakuwa ni kutenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Kwa hiyo, hata wewe upo katika sehemu ya mpango kwa sababu ndiyo jukumu kubwa tulilonalo sasa hivi. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved