Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 22 Water and Irrigation Wizara ya Maji 252 2026-05-05

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Primary Question

MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO aliuliza: -

Je, lini mradi wa maji kutoka Kisarawe Mjini kwenda Kata za Kazimzumbwi, Masaki, Msimbu, Kibuta hadi Marumbo utaanza kujengwa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Selemani Saidi Jafo, Mbunge wa Kisarawe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa kufikisha huduma ya maji safi na salama kwenye kata tano za Kazimzumbwi, Masaki, Msimbu, Kibuta pamoja na Marumbo zilizopo Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Miongoni mwa kazi zinazotarajiwa kutekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kupokea na kusukuma maji, ujenzi wa matanki mawili yenye jumla ya ujazo wa lita 800,000 sambamba na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 52.1.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo ambapo unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 13. Ahsante.