Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Primary Question
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO aliuliza: - Je, lini mradi wa maji kutoka Kisarawe Mjini kwenda Kata za Kazimzumbwi, Masaki, Msimbu, Kibuta hadi Marumbo utaanza kujengwa?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, mradi huu ni wa kimkakati na nimpongeze sana Waziri wa Maji, ndugu yangu Jumaa Aweso, aliweza kufika katika eneo hili la mradi.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini eneo hilo wananchi wana changamoto kubwa sana ya maji. Ukitoka pale Kazimzumbwi, Kisanga, Masaki, Kauzeni, Kibuta, Marumbo, Chang’ombe B, Chang’ombe A na huko eneo la Msimwa hali ni mbaya sana. Sasa nini kauli ya Serikali kuiagiza DAWASA kuanza kazi hiyo awamu kwa awamu? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ninaishukuru tena Wizara ya Maji, ilianza mradi wa maji Kijiji cha Chakenge ambao umefikia 75% na Kijiji cha Nyani karibu 98% lakini wakandarasi hao wote hawajalipwa hata senti tano mpaka hivi sasa na wamewasilisha certificate zao. Nini mpango wa Serikali kulipa hizo certificates? Lengo kubwa ni kwamba kazi hiyo iweze kukamilika wananchi waweze kupata maji. Ahsante. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Selemani Saidi Jafo, Mbunge mahiri kabisa kutoka Jimbo la Kisarawe ambaye ni sauti ya Wana-Kisarawe na hakika sisi Wizara ya Maji tunaendelea kushirikiana naye vizuri kwa hoja zake za wananchi na kwa kuwatetea wananchi wake na kwa kutimiza na kufuatilia vizuri falsafa ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani. Kwa hiyo, tunamshukuru sana Mheshimiwa Jafo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimejibu katika majibu yangu ya msingi, kazi ya upembuzi yakinifu imeshakamilika, usanifu wa kina umekamilika na usanifu huo ndiyo umetupa hii gharama ya shilingi bilioni 13. Hii kazi imeshaisha Mheshimiwa Selemani Jafo, hii kazi iliyobaki ni ndogo sana ambayo ni ya kutafuta fedha kama ambavyo nimejibu kwenye jibu la msingi ili sasa mradi uende kukamilika, na ninawaelekeza DAWASA, fedha zitakapopatikana, mradi huu uanze mara moja bila kuchelewa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua maeneo ya Masaki, Msimbu, Kibuta pamoja na Marumbo ndiyo kipaumbele cha Mheshimiwa Jafo, na sisi tutasimama kuhakikisha kwamba maeneo haya yanaenda kutekelezewa mradi ili waweze kupata huduma ya maji safi na salama. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala la pili, kama ambavyo nimesema kwamba Mheshimiwa Jafo anaendelea kufuatilia kwa ukaribu sana miradi hii, Mradi wa Chakenge aliousema uko 75%, Mradi wa Mafizi uko 98%, lakini ninatambua alishakutana na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na akawasilisha hata hati zile za madai.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninamhakikishia Katibu Mkuu wetu Wizara ya Maji Engineer Mwajuma analifanyia kazi na liko katika kipaumbele cha kuhakikisha kwamba wakandarasi hao wanalipwa ili waweze kukamilisha mradi ambao umefikia hatua nzuri kabisa. Nakushukuru sana. (Makofi)
Name
Kijakazi Mohamed Yunus
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO aliuliza: - Je, lini mradi wa maji kutoka Kisarawe Mjini kwenda Kata za Kazimzumbwi, Masaki, Msimbu, Kibuta hadi Marumbo utaanza kujengwa?
Supplementary Question 2
MHE. KIJAKAZI Y. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa usambazaji maji Liwale Mjini ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2024 kwa ahadi ya kukamilika mwaka 2025, mpaka sasa haujakamilika kwa sababu ya uhaba wa pesa. Katika shilingi bilioni 6.9 zimekwenda shilingi milioni 400 tu. Je, ni nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba wanapeleka pesa ili mradi ule uweze kukamilika na kuwaondolea adha ya maji wananchi wa Liwale hususan akina mama? Ahsante. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, miradi hii hakuna utakaosimama. Tunachokifanya ni kuhakikisha kwamba tunaweka mkakati wa kwenda awamu kwa awamu. Tunayo miradi kama ambavyo tumekuwa tukisema, miradi ambayo imefikia hatua nzuri 90%, 85% ni lazima tuitoe itoe matokeo halafu tunakuja katika miradi.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua mradi huo ni muhimu sana na wa kimkakati katika eneo hilo. Nakuhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tunaenda kuweka msukumo wa kutosha kwa kupeleka fedha katika mradi huo ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama utakapokamilika, lakini tunafahamu kwamba hatuwezi kutoa fedha kwa miradi yote inayoendelea nchi nzima ambayo yapata miradi 867 ambapo tukaweza kutoa pesa kwa pamoja.
Kwa hiyo, ni lazima tukibaliane tuwe na subira kidogo, tutaenda awamu kwa awamu, tutapeleka fedha awamu kwa awamu na mradi utaweza kukamilika bila kuwa na changamoto yoyote. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Christina Solomon Mndeme
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO aliuliza: - Je, lini mradi wa maji kutoka Kisarawe Mjini kwenda Kata za Kazimzumbwi, Masaki, Msimbu, Kibuta hadi Marumbo utaanza kujengwa?
Supplementary Question 3
MHE. CHRISTINA S. MNDEME: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi hii.
Kwa kuwa Serikali imetuletea Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria Mkoa wa Tabora na hivyo kwa kiasi kikubwa kutupunguzia adha ya maji ambayo tumekuwa nayo kwa kipindi kirefu sana ndani ya Mkoa wa Tabora, na kwa kuwa mradi huu bado haujafika katika maeneo mengi na hususan vijijini na waathirika wakubwa ni wanawake na wasichana waliopo maeneo ya vijijini mkoani Tabora.
Je, Serikali ina mpango gani wa kufikisha maji haya kutoka Ziwa Victoria katika maeneo mengi na hususan ya vijijini ambapo bado hawajafikiwa na mradi huu? Ahsante.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Christina Mndeme, Mbunge Viti Maalum kutoka Mkoa wa Tabora.
Mheshimiwa Naibu Spika, natambua kwamba anaendelea kufanya kazi aliyotumwa na wanawake wa Tabora, tunakushukuru sana na nakuhakikishia Wizara ya Maji chini ya Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso tutakupa ushirikiano kuhakikisha kwamba unafikia malengo ya kuwatumikia wanawake wa Tabora.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Ziwa Victoria kwa Tabora uko katika awamu mbalimbali, tunao mradi ambao ulikuwa na zaidi ya shilingi bilioni 680 kutoka Mwanza, Iherere pale, umepita Kahama, umeenda Nzega, umeenda Igunga mpaka huku Shelui, lakini tunayo awamu ya pili ambayo tunatoka Tabora, tunaenda Sikonge, tunaenda Urambo, tunaenda Kaliua, package ambayo ni ya zaidi ya shilingi bilioni 143. Nimtoe hofu, baada ya kujenga njia ya bomba kuu na kukamilika, baada ya hapo tutatekeleza Sera ya Wizara ya Maji ya kuhakikisha kwamba vijiji vyote, kilometa 12 kushoto na kulia wanapata huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Naibu Spika, na tukibaini baada ya kufanya hivyo kuna vijiji vimebaki, tutafanya usanifu mwingine wa kuhakikisha kwamba vijiji vyote vinafikiwa na huduma ya maji safi na salama yanatokana na Ziwa Victoria. Nakushukuru sana. (Makofi)
Name
Isack Joseph Copriano
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Monduli
Primary Question
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO aliuliza: - Je, lini mradi wa maji kutoka Kisarawe Mjini kwenda Kata za Kazimzumbwi, Masaki, Msimbu, Kibuta hadi Marumbo utaanza kujengwa?
Supplementary Question 4
MHE. ISACK J. COPRIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Nataka kujua Mradi wa kutoka Monduli Mjini – Monduli Juu - Maerete hadi kwa Hayati Edward Moringe Sokoine, mradi ambao unafanywa kwa force account. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha ili mradi huo uendelee ambao umekwama pale msituni?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Isack Copriano, Mbunge kutoka Monduli, kama ifuatavyo. Namshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji mzuri na ule mradi wako kutoka Ngaramtoni kuelekea Monduli wa vijiji 13 tunaendelea vizuri na mabomba yapo vizuri kabisa yanaendelea kuzalishwa, lakini nakutoa hofu, huu mradi ambao unatekelezwa kwa force account, huu hauna tatizo lolote, tunauweza kwa sababu unatekelezwa na wataalamu wetu wa ndani.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimtoe hofu, Katibu Mkuu atapeleka fedha na wataalamu wetu ambao ni mainjinia mahiri kabisa kutoka Wizara ya Maji wataukamilisha huu mradi bila kuwa na changamoto yoyote. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Chief Thomas Mgonto Kitima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ikungi Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO aliuliza: - Je, lini mradi wa maji kutoka Kisarawe Mjini kwenda Kata za Kazimzumbwi, Masaki, Msimbu, Kibuta hadi Marumbo utaanza kujengwa?
Supplementary Question 5
MHE. THOMAS M. KITIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii na mimi kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa tunavyozungumza ni takribani wiki ya nne wananchi wa Kata ya Mang’onyi katika Jimbo la Ikungi Mashariki hawana maji kabisa, na sababu kubwa ni kwamba motor imeungua na pa kubadilishwa mpaka iende Dar es Salaam. Je, Serikali inatoa kauli gani kwa watu hawa wa Mang’onyi ili waweze kupata huduma ya maji kwa haraka? Ahsante sana.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Mheshimiwa Mbunge hujasikika vizuri, naomba utaje hilo eneo ambalo maji yamekatika kwa muda ili Mheshimiwa Naibu Waziri asikie.
MHE. THOMAS M. KITIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa tunavyoongea ni takribani wiki ya nne wananchi wa Kata ya Mang’onyi katika Jimbo la Ikungi Mashariki hawana huduma ya maji, na sababu ambayo inazungumzwa ni ile motor kwamba imeungua na ili ibadilishwe lazima ipelekwe Dar es Salaam.
Je, Serikali inatoa kauli gani ili hawa watu wa Mang’onyi waweze kupata maji ukizingatia ni kwamba ni kata ambayo ina wawekezaji wakubwa ambao wanasaidia maendeleo katika Jimbo zima la Ikungi Mahariki?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na namshukuru sana kaka Mheshimiwa Thomas, Mbunge kutoka Ikungi kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa changamoto hii na kwa Serikali hii ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tatizo dogo la motor haliwezi kuwafanya Watanzania wakose huduma ya maji safi na salama. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, napenda kutumia fursa hii kumwelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji, hili suala alifuatilie haraka sana ili wananchi hawa waweze kupata huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Wizara ya Maji hatuwezi kushindwa kutekeleza jambo dogo kama hilo. Nimtoe hofu, hili jambo tumelipokea na tutalifanyia kazi na uhesabu kwamba hili tatizo limeisha. Ahsante sana. (Makofi)