Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 14 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 170 2026-04-22

Name

Yannick Ikayo Ndoinyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Primary Question

MHE. YANNICK I. NDOINYO aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Barabara kutoka Kigongoni hadi Wasso – Ngorongoro kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Yannick Ikayo Ndoinyo, Mbunge wa Ngorongoro, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Barabara ya Kigongoni ama Mto wa Mbu – Wasso – Loliondo yenye urefu wa kilometa 211 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa ujenzi kwa kiwango cha lami kwa Sehemu ya Wasso – Sale kilometa 49 umekamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mkataba wa ujenzi kwa sehemu ya Wasso – Loliondo urefu wa kilometa 10 umesainiwa, ambapo taratibu za malipo ya awali kwa mkandarasi zinaendelea. Vilevile, taratibu za manunuzi ya kuwapata wakandarasi wa ujenzi sehemu za Mto wa Mbu – Selela kilometa 23 na Selela – Engaruka kilometa 27 zinaendelea. Kwa sehemu zilizobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi, ahsante.