Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 15 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 171 2026-04-23

Name

Mwantatu Mbarak Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. MWANTATU M. KHAMIS aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Shule za Sekondari zinaondokana na Upungufu wa Vifaa vya Maabara?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantatu Mbarak Khamis, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikitoa fedha za ununuzi wa vifaa vya maabara kwa ajili ya ujifunzaji na ufundishaji wa masomo ya sayansi ili kuwa na wahitimu wenye umahiri unaoendana na zama za sayansi na teknolojia.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imetumia shilingi bilioni 3.51 kununua na kusambaza kemikali na vifaa vya maabara katika shule za sekondari 231. Vilevile, Serikali hivi sasa inaendelea na mchakato wa manunuzi yenye thamani ya shilingi bilioni 13.97 kwa ajili ya vifaa vya maabara vya shule 672.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha za ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule za sekondari ili kuboresha mazingira ya kujifunza na ufundishaji wa masomo ya Sayansi.