Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwantatu Mbarak Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. MWANTATU M. KHAMIS aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Shule za Sekondari zinaondokana na Upungufu wa Vifaa vya Maabara?

Supplementary Question 1

MHE. MWANTATU M. KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, ningependa kumwuliza swali lenye kipengele (a) na (b) la nyongeza:-

(a) Kuna mpango gani wa Serikali katika kuhakikisha shule za wasichana zinazojengwa mikoani zinapatiwa vifaa vya maabara vya kutosha pamoja na watu wa maabara?

(b) Kwa kuwa Serikali inaendelea kujenga majengo ya shule za sekondari, je, ni upi mkakati wa Serikali katika kuhakikisha changamoto hii inapatiwa mwarobaini wake?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Serikali kwanza imeweka kipaumbele cha hali ya juu katika ujenzi wa shule za masomo ya sayansi, na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imejenga shule za sayansi za mikoa 26 kwa kila mkoa ambazo ziligharimu takribani shilingi bilioni 4.6 kila shule.

Mheshimiwa Naibu Spika, shule zile zimejengewa miundombinu yote kwa maana ya maabara za Fizikia, Kemia na Biolojia, na zimepelekewa vifaa vya maabara na wataalamu wa maabara ili kuwezesha masomo ya sayansi yaweze kufanyika kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaomba nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaendelea kutenga fedha. Hivi sasa tuko kwenye taratibu za manunuzi ya vifaa vya maabara vya zaidi ya shilingi bilioni 13.97 ili kuhakikisha shule zetu zote za wasichana, shule za wavulana na shule mchanganyiko zinapata vifaa vya kutosha vya maabara ili wanafunzi wetu waweze kusoma vizuri na kwa ufanisi zaidi. Ahsante.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTATU M. KHAMIS aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Shule za Sekondari zinaondokana na Upungufu wa Vifaa vya Maabara?

Supplementary Question 2

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Jimbo la Bunda Mjini linahitaji maabara 48 na maboma ya maabara 13. Ni lini mtatusaidia kukamilisha hili ili na sisi tutoe wataalamu wa sayansi katika jimbo la Bunda Mjini?




Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeweka mpango mzuri na madhubuti wa kuhakikisha maeneo yote ya shule zetu za sekondari yenye upungufu wa majengo ya maabara au yenye maabara ambazo hazijakamilishwa, tunakamilisha maabara hizo na tunajenga maabara na kupeleka vifaa na wataalamu ili kuhakikisha watoto wetu wanasoma masomo ya sayansi katika mazingira bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mtaala wa Elimu wa Mwaka 2014, Toleo la 2023, ambapo tumeanzisha utaratibu wa shule za amali pamoja na kuboresha sana eneo la shule za masomo ya sayansi, tumeweka mkakati ambao nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi karibuni baada ya taratibu kukamilika tutakuwa na mpango kabambe wa kuboresha miundombinu ya elimu ya sayansi kwa maana ya kujenga maabara hizo na kukamilisha pia elimu ya mafunzo ya amali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge kwamba Serikali iko makini na tutahakikisha tunatekeleza suala hilo.

Name

Alan Thomas Mvano

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kakonko

Primary Question

MHE. MWANTATU M. KHAMIS aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Shule za Sekondari zinaondokana na Upungufu wa Vifaa vya Maabara?

Supplementary Question 3

MHE. ALAN T. MVANO: Mheshimiwa Naibu Spika, Shule tatu za sekondari katika Jimbo la Kakonko hazina kabisa vyumba vya maabara, nazo ni Kambi Secondary, Dr. Mpango Secondary na Kakonko Boys Secondary School. Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha shule hizi tatu nazo zinapata maabara? Ahsante sana.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Alan Mvano, Mbunge wa Kakonko, alishaleta taarifa hiyo Ofisi ya Rais, TAMISEMI, na tayari Idara ya Elimu imeshaandaa mpango kwa ajili ya kuanza ujenzi wa maabara hizo katika shule za sekondari tatu. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itafanya shughuli hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii pia kumsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kwamba pamoja na fedha za Serikali Kuu, ni muhimu waanze hatua za awali za ujenzi kwa awamu kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ili fedha za mapato ya Serikali Kuu zikienda zifanye umaliziaji wa majengo ya maabara hizo.

Name

Sara Msafiri Ally

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. MWANTATU M. KHAMIS aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Shule za Sekondari zinaondokana na Upungufu wa Vifaa vya Maabara?

Supplementary Question 4

MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ni ahadi ya Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi kujenga maktaba na maabara ya kisasa kwenye kila wilaya. Je, ni lini Serikali itajenga maabara na maktaba ndani ya Jimbo la Mvomero?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ni Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, na ni dhamira ya Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya maktaba na maabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Sara Msafiri, Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Serikali inaendelea hivi sasa na ujenzi katika maeneo mbalimbali kote nchini, lakini kwa sababu uhitaji ni mkubwa, Serikali inaendelea kuratibu upatikanaji wa fedha na tutaendelea kujenga miundombinu hiyo kwa awamu. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba pia Jimbo la Mvomero litapewa kipaumbele.

Name

Fadhili Sandali Chilombe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. MWANTATU M. KHAMIS aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha Shule za Sekondari zinaondokana na Upungufu wa Vifaa vya Maabara?

Supplementary Question 5

MHE. FADHILI S. CHILOMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Katika Jimbo la Tunduru Kusini kuna Sekondari ya Tuwemacho na Masakata, Mtina na Mchoteka, zote hizi tayari zimeshakamilika, zina maabara, lakini hazina vifaa. Nini kauli ya Serikali kupeleka vifaa kwenye shule hizo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini kwamba kama alivyosema Serikali tayari imekamilisha ujenzi wa maabara katika shule hizo tatu na hiyo ilikuwa ni hatua ya kwanza, hatua ya pili ambayo tutakwenda kuhakikisha inatekelezwa ni kupeleka vifaa vya maabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, na katika kipindi hiki ninachoongea hapa tayari tuna taratibu za manunuzi ya vifaa vya maabara vya zaidi ya shilingi bilioni 13.97 na mara baada ya kukamilika taratibu hizo tutahakikisha shule hizo pia zinapewa kipaumbele kupelekewa vifaa vya maabara ili watoto wetu waweze kupata mazingira bora zaidi ya kujifunza.