Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 11 | Sitting 15 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 173 | 2026-04-23 |
Name
Khalid Mussa Nsekela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. KHALID M. NSEKELA aliuliza: -
Je, lini Serikali itachukua hatua za haraka za upatikanaji wa maji safi na salama katika Zahanati, Vituo vya Afya, Masoko na Mashuleni – Kyerwa?
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Khalid Mussa Nsekela, Mbunge wa Jimbo la Kyerwa kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha inafikisha huduma ya majisafi na salama kwenye maeneo yote yanayotoa huduma za kijamii ikiwemo shule, vituo vya kutolea huduma za afya, vituo vya mabasi na masoko. Huduma hiyo imeshapatikana kwenye baadhi ya maeneo mbalimbali nchini kupitia miradi ya maji iliyopo, sambamba na ile inayoendelea kujengwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia mwezi Machi, 2026, Serikali imefikisha huduma ya majisafi na salama kwenye shule 9,957 na vituo 4,348 vya kutolea huduma za afya kote nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Wilaya ya Kyerwa, Serikali imefikisha huduma ya majisafi na salama kwenye Shule za Msingi na Sekondari 55 na Vituo 18 vya kutolea huduma za Afya pamoja na Hospitali ya Wilaya. Serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha kipekee kwenye maeneo yote yanayotoa huduma za kijamii ili kuhakikisha yanafikiwa na huduma ya majisafi na salama kadiri miradi ya maji inavyotekelezwa kwenye maeneo yote nchini ikiwemo Wilaya ya Kyerwa.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved