Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Khalid Mussa Nsekela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. KHALID M. NSEKELA aliuliza: - Je, lini Serikali itachukua hatua za haraka za upatikanaji wa maji safi na salama katika Zahanati, Vituo vya Afya, Masoko na Mashuleni – Kyerwa?
Supplementary Question 1
MHE. KHALID M. NSEKELA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, je, kwa kuwa Wilaya ya Kyerwa imekuwa na changamoto ya muda mrefu ya huduma ya maji, Serikali haioni haja ya kuifanya Wilaya ya Kyerwa kuwa kanda maalum ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maji?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuambatana na mimi na kufika Kyerwa kujionea changamoto ya maji iliyokuwa? Ahsante sana.
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge. Kwa kweli moja ya ajenda yake katika Bunge hili ni kuhusu suala zima la Wanakyerwa kuweza kupata huduma ya majisafi na salama. Sisi kama Wizara ya Maji ni wilaya ambayo tumeiangalia kwa kina sana. Ni moja ya wilaya tulizoifanyia tathmini, hasa katika kipindi hiki kwamba ni wilaya ambayo ina vijiji takribani 99, tumeshafikisha zaidi ya vijiji 55. Ipo miradi ya kimkakati ambayo tunaitekeleza katika kuhakikisha wananchi wa Kyerwa wanapata huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunao mradi wa Runyinya-Chanya zaidi ya shilingi bilioni 3.7, Kimuli-Nyanga zaidi ya shilingi bilioni mbili, Kaisho-Isingiro zaidi ya shilingi bilioni 1.9. Ninataka niwahakikishie, tutaisimamia Wanakyerwa waweze kupata huduma ya majisafi na salama, na mimi baada ya Bunge nipo tayari kuongozana na wewe kufika katika jimbo lako la Kyerwa. Ahsante sana.
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. KHALID M. NSEKELA aliuliza: - Je, lini Serikali itachukua hatua za haraka za upatikanaji wa maji safi na salama katika Zahanati, Vituo vya Afya, Masoko na Mashuleni – Kyerwa?
Supplementary Question 2
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Halmashauri ya Mji Njombe tuna mradi wa Igombwi umekaa zaidi ya miaka sita bila kukamilika, uko 85%. Ninaomba uhakika ni lini mradi huu utakamilika? Je, umetengwa kwenye bajeti ya sasa?
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa swali hili. Huo ni mradi wa kimkakati, na ni moja ya agenda katika jimbo lake. Tumepokea zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya malipo ya wakandarasi. Tutatoa fedha kuhakikisha mradi unakamilika na wananchi hawa waweze kupata huduma ya majisafi na salama.
Name
Innocent Lugha Bashungwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karagwe
Primary Question
MHE. KHALID M. NSEKELA aliuliza: - Je, lini Serikali itachukua hatua za haraka za upatikanaji wa maji safi na salama katika Zahanati, Vituo vya Afya, Masoko na Mashuleni – Kyerwa?
Supplementary Question 3
MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Wanavijiji wa vijiji vya Nyakakika, Kanogo, Omukakajinja, Janyanatika na Kanyamaganda, kwanza wanampongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuri anayoifanya, lakini wanamlilia na kuomba mtambo wa kuchimba visima katika hivi vijiji. Je, anawaambiaje wananchi hawa?
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli ninampongeza Mheshimiwa Mbunge. Nimwambie tu, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameapa kumtua mwanamke ndoo kichwani. Katika jitihada zake za dhati amenunua mitambo kwa ajili ya uchimbaji visima katika kila mkoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mitambo yetu ipo karibu, lakini hayo maeneo ambayo ameyaeleza tutayapangia nguvu na kuhakikisha kwamba mtambo unafika na wanachimbiwa visima na watu waweze kupata huduma ya majisafi na salama.
Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. KHALID M. NSEKELA aliuliza: - Je, lini Serikali itachukua hatua za haraka za upatikanaji wa maji safi na salama katika Zahanati, Vituo vya Afya, Masoko na Mashuleni – Kyerwa?
Supplementary Question 4
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo langu la Same Mashariki lina kata kubwa mbili. Kata ya Maore ina takribani watu 20,000 na Kata ya Ndungu ina takribani watu 19,000. Kata hizi miradi yake yote ni ya mwaka 1967 na kwa sasa hivi wana shida kubwa sana. Mheshimiwa Waziri alifika jimboni kwangu, ananiambia nini sasa kuhusu kata hizi mbili asubuhi hii?
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie Mheshimiwa Mbunge, kwa kuwa tunakwenda kwenye bajeti, na bajeti yetu ni tarehe tano na tarehe sita, niombe saa saba tukutane, tuone namna tunavyojipanga ili kuweza kuwasaidia wananchi wake, ahsante sana.
Name
Moses Ludovico Kaegele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkasi Kusini
Primary Question
MHE. KHALID M. NSEKELA aliuliza: - Je, lini Serikali itachukua hatua za haraka za upatikanaji wa maji safi na salama katika Zahanati, Vituo vya Afya, Masoko na Mashuleni – Kyerwa?
Supplementary Question 5
MHE. MOSES L. KAEGELE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Wazir, Kata ya Myula yenye vijiji vitano, ndani ya vijiji vinne vyote hamna maji safi na salama lakini Shule ya Sekondari ya Myula nayo haina maji safi na salama. Ni upi mpango wa Serikali wa dharura wa kupeleka maji safi na salama katika Shule ya Sekondari ya Myula?
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka niwahakikishie Wabunge na nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa ajenda yake hii ya maji. Ninataka nimhakikishie tumejipanga vizuri kwenye bajeti yetu maeneo ambayo nchi nzima ambapo hatujafikisha maji ni vijiji 1,575. Kwa hiyo, mkakati wetu wa Wizara ya Maji ni kuhakikisha bajeti hii katika kipindi cha miaka mitano vijiji vyote ambavyo vimebaki vinakwenda kupata huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. KHALID M. NSEKELA aliuliza: - Je, lini Serikali itachukua hatua za haraka za upatikanaji wa maji safi na salama katika Zahanati, Vituo vya Afya, Masoko na Mashuleni – Kyerwa?
Supplementary Question 6
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Sekondari ya Kata ya Nanyala imekuwa haina maji kwa muda mrefu na ni sekondari ya kidato cha kwanza mpaka cha sita. Ni lini mkandarasi aliyepewa kupeleka maji katika shule hiyo atarudi kazini ili aweze kupeleka maji kwenye shule hiyo?
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mkandarasi yupo na anatekeleza mradi ninadhani kuna haja ya kumwongezea nguvu na kumpatia fedha. Nipo tayari kuwapatia fedha kuhakikisha mradi unakamilika na shule hii iweze kupata huduma ya maji safi na salama.