Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2000-2005 | Session 12 | Sitting 15 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 175 | 2026-04-23 |
Name
George Natany Malima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara kutoka Njiapanda ya Kongwa hadi Mpwapwa Mjini kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kongwa – Mpwapwa yenye urefu wa kilometa 38.45 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa 6.45 zimejengwa kwa kiwango cha lami kuanzia Mpwapwa Mjini hadi Mwanakianga. Aidha, mkataba wa ujenzi kwa sehemu iliyobaki ya kuanzia Mwanakianga – Kongwa (urefu wa kilometa 32) umesainiwa ambapo taratibu za malipo ya awali kwa Mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi zinaendelea.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved