Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara kutoka Njiapanda ya Kongwa hadi Mpwapwa Mjini kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya serikali, nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa mkandarasi huyu amekuwepo site kwa zaidi ya miaka miwili sasa na kumezuka uvumi kwamba huyu siyo yule anayetarajiwa kujenga hii barabara isipokuwa yeye ni mfanyabiashara wa kokoto tu. Hii inatokana na ukweli kwamba wananchi wamekuwa wakiona malori yakibeba kokoto inayotengenezwa katika site hiyo na kupelekwa maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ili kuondoa sintofahamu hii, Serikali inawaambia nini wananchi wa Mpwapwa kuhusu uvumi huu ambao umezagaa katika Jimbo la Mpwapwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Mpwapwa lakini pamoja na wananchi wa jimbo lake kwamba mkandarasi huyu ambaye ni SG ni kati ya wakandarasi naweza nikasema kati ya wakandarasi bora wazawa katika nchi ya Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunapoongea sasa hivi huyu mkandarasi ndiye anayejenga barabara ya kule Kigamboni - Kibada kwenda Mwasonga kilometa 41. Lakini mkandarasi huyu ndiye aliyejenga njia nne za Kimara kwenda Kibaha. Mkandarasi huyu pia ndiye amejenga ile pale tulipokuwa tunakwama sana eneo la Mtanana, nadhani wote tunapita Mtanana.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niwahakikishie waheshimiwa wananchi wa Mpwapwa na Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi tunaamini kati ya wakandarasi bora ni huyu na nadhani nimetaja barabara chache ambazo amezijenga nadhani zinaweza zikapimwa na ubora wake. Kwa hiyo, niwahakikishie wana Mpwapwa na Mheshimiwa Mbunge kwamba kinachosubiriwa alipwe advance na hakika mtaelewa kwamba huyu ni mkandarasi ambaye ni bora kabisa.

Name

Anton Albert Mwantona

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rungwe

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara kutoka Njiapanda ya Kongwa hadi Mpwapwa Mjini kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri Mkuu alifanya ziara katika jimbo langu la Rungwe akaahidi kwamba barabara kutoka KK kuelekea Kafwafwa kule Ileje na barabara kutoka Kiwira kuelekea Isangati maandalizi yaanze kufanyika kwa kuijenga kiwango cha lami. Je, ni lini barabara hizi zitaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?


Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. KK kwenda Kafwafwa inakamilishwa usanifu na kutoka Kiwira kwenda Isangati barabara hiyo ipo kwenye mpango sasa wa kuanza kusanifiwa kwa sababu ilikuwa bado haijasanifiwa.

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara kutoka Njiapanda ya Kongwa hadi Mpwapwa Mjini kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa Serikali ina mpango wa kuanza ujenzi wa barabara ya Makofia-Mlandizi; je, lini sasa wananchi wa kata ya Yombo watalipwa fidia zao? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Barabara ya Makofia-Mlandizi ilikuwa imeshafanyiwa uthamini siku za nyuma lakini muda wake ulikuwa umeshapita, na tumeshafanya uthamini upya kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kuwalipa na tunapoongea sasa hivi majedwali ya fidia ya wananchi hao yako hazina kwa ajili ya kupata fedha ili waweze kulipwa hiyo fidia na barabara ijengwe ya kuunganisha Bagamoyo na Mlandizi.

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara kutoka Njiapanda ya Kongwa hadi Mpwapwa Mjini kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 4

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ilitujengea barabara kutoka Tosamaganga kwenda kijiji cha Ugwachanya, bahati mbaya kuna mita kama 900 zimebaki sasa ni miaka mitatu. Je, Serikali itatumalizia lini hicho kipande cha mita 900 kati ya Tosamaganga na kijiji cha Ugwachanya?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba aweze kurudia ninaomba Mheshimiwa Mbunge niweze kuelewa vizuri kipande hicho cha barabara alichokitaja.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kiswaga, taja barabara hiyo hajasikia vizuri Mheshimiwa Naibu Waziri.

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi mara ya pili. Nasema hivi, Serikali ilitujengea barabara kutoka kijiji cha Tosamaganga kwenda kijiji cha Ugwachanya lakini barabara hiyo haijakamilika kwa kipande cha mita kama 900 huu ni mwaka wa tatu. Je, ni lini sasa Serikali itamalizia kipande hicho kilichobaki?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue suala hili la Mheshimiwa Mbunge na niweze kujiridhisha baada ya kuwasiliana na wenzetu wa Mkoa wa Iringa changamoto ya hicho kipande kilichobaki ni nini halafu nitampa majibu sahihi Mheshimiwa Mbunge na nini mpango wa Serikali katika hicho kipande ambacho kimebaki.