Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 39 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 458 2026-05-29

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea ambayo inategemewa na wananchi wengi?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala, Katiba na Sheria, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni moja ya hospitali 25 zilizoanza ujenzi katika awamu ya tatu, mwaka wa fedha 2021/2022. Mpaka sasa hospitali hiyo imepokea jumla ya shilingi bilioni 2.6 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Kuhudumia Wagonjwa Nje (OPD), Jengo la Maabara, Jengo la Mionzi, Jengo la Utawala, Jengo la Wazazi, Jengo la Kufulia na Jengo la Kuhifadhia Dawa. Aidha, Hospitali ya Manispaa ya Songea imeanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje (OPD) na vipimo mwaka 2023.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali imetenga shilingi milioni 750 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya watoto, wodi ya magonjwa ya ndani wanaume na wanawake, pamoja na store ya chanjo katika Hospitali ya Manispaa ya Songea. Ninaomba kuwasilisha.