Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Songea Mjini

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea ambayo inategemewa na wananchi wengi?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Naibu Waziri, Mheshimiwa Jafar kwa majibu haya mazuri yenye kuleta matumaini kwa Wana-Songea. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, kwa kuwa Mji wa Songea ni mmoja ambao unakuwa kwa kasi, hasa ongezeko la idadi ya watu. Nini mpango wa Serikali kupanua huduma hususan huduma za madaktari bingwa katika hospitali hiyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kwamba kwa kuwa Mji wa Songea unazidi kupanuka, idadi ya watu inavuka 500,000 kwa hivi sasa na katika hospitali hiyo kuna ambulance moja tu. Nini mpango wa Serikali wa kuongeza idadi ya ambulance katika hospitali hiyo? (Makofi)

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro, Mbunge wa Songea Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Afya kwenye huduma za kibingwa, kwanza tuko katika level za hospitali zote za mikoa, Regional Referral Hospitals na katika hospitali za wilaya baadhi ambazo tunaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa tutaendelea kufanya mawasiliano na wenzetu wa Wizara ya Afya ili kuona ni namna gani tunaanza huduma za kibingwa katika hospitali yetu hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika halmashauri yetu hii, angalau kwa awamu ya kwanza waliweza kupata ambulance mbili, lakini namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kwa maana amewaombea wananchi hawa na idadi ni kubwa na anakidhi vigezo, kwa maana ya kwamba halmashauri zile za pembezoni zitaangalia ni namna gani ambulance zile ambazo tunazipokea kutoka Wizara ya Afya tuweze kumuongezea na wananchi waweze kupata huduma hii bora kabisa ya kuhudumia mama na ndugu zetu katika maeneo hayo. Ninaomba kuwasilisha. (Makofi)

Name

Johannes Lembulung’ Lukumay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea ambayo inategemewa na wananchi wengi?

Supplementary Question 2

MHE. JOHANNES L. LUKUMAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali na ninachukua nafasi hii kumshukuru kabisa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutoa shilingi bilioni 5.5 iliyosababisha kujengwa na kumalizika kwa vituo vitano vya afya katika Jimbo la Arumeru Magharibi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hivyo vituo vitano, vinne vinatoa huduma ya upasuaji, hususan upasuaji wa mama wajawazito, lakini vituo vitatu havina nyumba za watumishi kabisa, inayosababisha watumishi wale wakae mbali zaidi na vituo vya afya.

Swali, je, lini Serikali itajenga nyumba za watumishi katika Kituo cha Afya cha Oldonyosambu, Mbuyuni, Oloirien na Nduruma ili wananchi hawa waende kupata huduma iliyokusudiwa? Ninashukuru sana.

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Lukumay, Mbunge na pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, imeeleza Bunge lako Tukufu ni namna gani approach ya kwanza ya kujenga nyumba za watumishi. Lengo hasa ni kuhakikisha zile halmashauri za pembezoni zenye uhitaji mkubwa tunaanza ujenzi wa nyumba za watumishi katika maeneo hayo ili waweze kutoa huduma bora na wapate utulivu. Ninaomba kuwasilisha.

Name

Esther Nicholas Matiko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea ambayo inategemewa na wananchi wengi?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Mji wa Tarime inahudumia wananchi wa Mji wa Tarime, Wilaya ya Tarime, wengine wanatoka Rorya na hata nchi jirani ya Kenya. Naishukuru Serikali kwa kutujengea jengo jipya kabisa la mama na mtoto, lakini bado kuna mahitaji ya huduma ya watoto wachanga au njiti, (Radiant Warmer, UT Warmer Baby Coat Five), pamoja na phototherapy machines.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali hiyo ni ya zamani, imechakaa, OPD ni mbovu kabisa na haifai, pamoja na jengo la utawala. Nataka kujua sasa ni lini Serikali itapeleka fedha, ili kuweza kujenga Jengo la OPD na la utawala kuweza kuendana na ukarabati wote ambao imeufanya wa EMD, hiyo maternity complex na vingine? (Makofi)

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ujumla pongezi ambazo Waheshimiwa Wabunge wamezitoa na zile ambazo Mheshimiwa Lukumay ametoa, hakika zinakwenda kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa maana ameweka fedha, ameweka nguvu yake yote katika kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora na tumeweza kupata heshima kimataifa kwamba Tanzania tunazidi kupambana kuzidi kupunguza tatizo la mama na mtoto. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Matiko kwamba tutaendelea kutenga fedha kuhakikisha tunajenga hizo wodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeweza kurekebisha zaidi ya hospitali 49 zile kongwe, kuhakikisha tunaweka miundombinu sawa. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Esther kwa mwaka huu wa fedha ambao tumeendelea kutenga, zaidi ya hospitali 105 zitapata fedha kati ya shilingi milioni 600, shilingi milioni 700 na shilingi milioni 800, kuhakikisha tunakamilisha miundombinu hii. Kwa hiyo, wananchi wale wataendelea kupata huduma na tutakamilisha OPD ambayo Mheshimiwa Esther ameiomba hapa. Ninaomba kuwasilisha. (Makofi)

Name

Anne Kilango Malecela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Same Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea ambayo inategemewa na wananchi wengi?

Supplementary Question 4

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, wakati Makamu wa Rais anapita kutafuta kura katika uchaguzi wa mwaka 2025 alitoa ahadi kwamba Serikali imeona ukubwa wa Wilaya ya Same kwa hiyo, imeamua kujenga Hospitali ya Wilaya upande wa Jimbo la Same Mashariki. Je, Serikali itaanza lini kuijenga hospitali hii kwa sababu sasa wananchi wanauliza mara kwa mara? Ahsante.

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Same, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kuhakikisha kwamba anafuatilia na kuona namna gani Serikali itaendelea kutimiza ahadi ambayo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliitoa. Ofisi ya Waziri Mkuu, tumesema katika Bunge lako Tukufu kwamba ahadi zote za viongozi wetu wakuu wa nchi tutahakikisha tunazitimiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri alete andiko, waanze kutenga eneo na tuanze ujenzi katika eneo hilo hata angalau kwa kutenga eneo ili tuweze kutenga bajeti ya kujenga angalau kwa awamu. Ninaomba kuwasilisha. (Makofi)

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea ambayo inategemewa na wananchi wengi?

Supplementary Question 5

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, Serikali imetujengea hospitali nzuri sana pale Nyamuswa, Bukama, lakini hospitali hiyo toka mwaka 2019 mpaka leo ina waganga watatu. Sasa ni lini Serikali itapeleka waganga na wahudumu kwenye hospitali ili ifanye kazi vizuri?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuajiri wataalamu katika hospitali zetu zote nchini na tunakumbuka ahadi ya Mheshimiwa Rais, tuliweza kupata vibali vya kuajiri wataalamu zaidi ya 5,000 katika hospitali zetu na wamesambazwa kote nchini. Tayari tunaendelea kuratibu, kuona upungufu katika maeneo mbalimbali ili tuendelee kuongeza watu. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Getere kwamba tutaendelea kuongeza watalaamu katika hospitali zetu hizi ili wananchi waweze kupata huduma ambayo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameikusudia. Ninaomba kuwasilisha.

Name

Alan Thomas Mvano

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kakonko

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea ambayo inategemewa na wananchi wengi?

Supplementary Question 6

MHE. ALAN T. MVANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, katika Wilaya ya Kakonko kipo Kituo cha Afya Mganza ambacho kipo karibu na Kakonko Mjini, kinahudumia Kata ya Kakonko, Kiziguzigu, Kanyonza, Kasuga na Lugenge. Ni upi mpango wa Serikali kuongeza gari la wagonjwa ili kuweza kuboresha huduma katika eneo la afya? Ahsante.

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama alivyouliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzuri Mheshimiwa Mbunge wa Kakonko tunafanya mawasiliano ya mara kwa mara, huwa anakuja kwenye dawati na pia pale Wizarani ili kuona namna gani tunaboresha huduma katika jimbo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kulingana na tunavyopokea magari kutoka Wizara ya Afya tutahakikisha tunaangalia, kwa sababu na yeye anaingia kwenye vipaumbele vya halmashauri ambazo ziko pembezoni na majimbo ambayo yako pembezoni ili waweze kupata huduma ya gari la wagonjwa. Ninaomba kuwasilisha.

Name

Mabula Johnson Magangila

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. DKT. DAMAS D. NDUMBARO aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Songea ambayo inategemewa na wananchi wengi?

Supplementary Question 7

MHE. MABULA J. MAGANGILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, wananchi wa Jimbo la Msalala, Kata ya Busangi na Kata ya Jana wanasafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma ya kituo cha afya na inasababisha akinamama wanajifungua njiani. Ni upi mpango wa Serikali kupeleka pesa na kujenga vituo vya afya kwenye hizi Kata za Busangi na Vyalo? (Makofi)

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Msalala, ndugu yangu huyu, njia moja nikiwa ninaelekea Jimboni Busanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba zile fedha ambazo tuliomba za vituo vya afya vya kimkakati, ukiacha vile 120 ambavyo tayari tumejenga, tayari tumeomba fedha Hazina ili kuhakikisha tunajenga vituo vya afya vya kimkakati na yeye ni mnufaika katika Jimbo hilo la Msalala ili kuweza angalau kujenga kituo cha afya cha kimkakati kitoe huduma kwa mama na ndugu zetu. Ninaomba kuwasilisha.