Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 39 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 459 2026-05-29

Name

Dougras Didas Massaburi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kivule

Primary Question

MHE. DOUGRAS D. MASSABURI aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa madaraja na Barabara ya Kitunda – Nyangasa – Kibeberu hadi Magole kwa kiwango cha lami?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dougras Didas Massaburi, Mbunge wa Jimbo la Kivule, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Kibeberu kwenda Magole ina urefu wa kilometa 2.89 na ni kiungo muhimu kwa wananchi wa Kata ya Mzinga na Kitunda. Katika mwaka wa fedha 2026/2027 barabara hii imejengwa kwa kiwango cha changarawe kwa gharama ya shilingi milioni 127.13. Serikali imekuwa ikitenga bajeti kuhakikisha Barabara za Kitunda – Nyangasa – Kibeberu hadi Magole zinapitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali imejikita katika ujenzi wa Barabara ya Kitunda – Mwangati – Kwa Mpalange ambapo katika bajeti ya mwaka 2026/2027 kiasi cha shilingi milioni 950 kimetengwa. Ujenzi wa Madaraja na Barabara za Nyangasa – Kibeberu na Magole itawekwa kwenye bajeti baada ya kukamilika kwa Barabara ya Kitunda – Mwangati - Kwa Mpalange. Ahsante.