Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 39 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 460 2026-05-29

Name

Abdulaziz Mohamed Abood

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Mjini

Primary Question

MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza: -

Je, lini tatizo la mafuriko Kata za Lukobe na Kihonda litamalizika ambapo wananchi wamekuwa wakiathirika na baadhi ya nyumba kubomoka?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdul-Aziz Mohamed Abood, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata za Kihonda na Lukobe katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro zimekuwa zikiathiriwa na mafuriko ya mara kwa mara nyakati za mvua. Ili kutatua changamoto hiyo, Serikali imepanga kujenga mfereji ili kuyaelekeza maji katika Mto Ngerengere. Serikali imeunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kufanya tathmini na kuandaa andiko la mradi ambalo litaonesha mahitaji halisi na njia nzuri ya kulifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, timu ya tathmini inatarajia kukamilisha kazi hiyo kabla au ifikapo Septemba, 2026.