Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 39 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 464 2026-05-29

Name

Martha Festo Mariki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga soko la kimataifa la mazao ya kilimo katika eneo la Majimoto, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa ujenzi wa masoko ya kimkakati ya mazao ya kilimo katika halmashauri mbalimbali nchini kwa lengo la kuendelea kuimarisha biashara ya mazao ya kilimo. Aidha, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Wizara imepanga kufanya tathmini ya ujenzi kwa maeneo yenye kipaumbele kulingana na vigezo vya uzalishaji wa mazao, wingi wa biashara ya mipakani, pamoja na upatikanaji wa rasilimali na mahitaji ya miundombinu ikiwemo eneo la Majimoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa Wizara ya Kilimo itafanya tathmini ya ujenzi wa soko hilo na utekelezaji wake utafanyiwa kazi kwa kuzingatia tathmini hiyo.