Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Martha Festo Mariki
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga soko la kimataifa la mazao ya kilimo katika eneo la Majimoto, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi?
Supplementary Question 1
MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali ambayo yanatoa matumaini kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi, hususan kwa wananchi wa eneo la Majimoto.
Kwa kuwa wananchi wa Mkoa wa Katavi ni wakulima wazuri sana wa mazao ya mpunga, mahindi, ufuta pamoja na tumbaku, upi mkakati wa Serikali sasa wa kuwatafutia masoko ya uhakika ili wananchi waweze kujipatia kipato, kwa kuwa wamekuwa wakilima vizuri, lakini kuna wakati soko la uhakika limekuwa likisumbua? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, dada yangu Mheshimiwa Martha Festo Mariki, ameuliza swali jema na la msingi na nimpe tu taarifa kwamba moja; soko la kwanza la mazao kama mahindi na mpunga hapa nchini ni kupitia Wakala wetu wa Taifa (NFRA).
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili NFRA kama sasa hivi tumefungua masoko nje ya nchi, tumefungua Kenya, Malawi na Congo, tunakwenda mpaka Misri sasa hivi na Zambia. Maeneo ambayo sasa tuna uhakika wa kuuza mazao yetu muda wote na imekuwa guaranteed hivyo. Kwa hiyo tu, nimthibitishie hilo ni soko namba moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, soko la pili tumeshaelekeza balozi zote nchini kuhakikisha kwamba wanafungua masoko katika hayo maeneo ili wananchi waweze kufikisha hayo mazao. Kwa hiyo, watu wa Katavi lakini na maeneo mengine hapa nchini watakuwa na uhakika wa kuuza masoko yao bila kuwazuia kwa kufuata sheria na taratibu ambazo tumeweka hapa nchini, ahsante.
Name
Thomas Maganga Kampala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Katavi
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga soko la kimataifa la mazao ya kilimo katika eneo la Majimoto, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi?
Supplementary Question 2
MHE. THOMAS K. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Waziri, unajua fika Jimbo la Katavi ni moja ya Jimbo ambalo linafanya vizuri kwenye kilimo cha mazao mchanganyiko. Pamoja na kufanya vizuri kwenye upande wa mazao, Jimbo la Katavi halina soko hata moja la mazao. Je, nini mkakati wa Serikali kujenga soko kwenye Jimbo la Katavi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninamthibitishia tu kaka yangu, Mheshimiwa Thomas Maganga Kampala, Mbunge wa Katavi, kama nilivyojibu katika swali la msingi kuwa yale maeneo ambayo tunakwenda kufanyia tathmini kulingana na vipaumbele ikiwemo uzalishaji mkubwa, ni pamoja na Jimbo la Katavi, lipo katika huo mpango. Tukishafanya maana yake hatua inayofuata ni ujenzi.
Name
Josephine Joseph Kapoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga soko la kimataifa la mazao ya kilimo katika eneo la Majimoto, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi?
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, wakazi wa Morogoro Vijijini wanaendelea kuishukuru Serikali kwa kuendelea kuliongezea thamani zao la karafuu. Hivi karibuni tumefanikiwa kufungua maghala matatu; Kinole, Tawa na Kisemu. Kwa msimu wa mwaka jana tu, tumepata zaidi ya shilingi bilioni ya 41.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunakuwa na Stakabadhi Ghalani ili tupate kuongeza thamani ya hili zao la karafuu? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze dada yangu Mheshimiwa Josephine Kapoma, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Morogoro kwa swali lake la msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri nipongeze Mkoa wa Morogoro kwa jitihada kubwa wanayoifanya sasa hivi ya kuzalisha karafuu kwa wingi na kutaka kuwa miongoni mwa maeneo ama mikoa itakayoongoza kwa uzalishaji hapa nchini. Ninafahamu na kwenye huo mkakati mimi mwenyewe nilikuwepo. Mkakati wa Serikali ni kwamba; cha kwanza tuongeze uzalishaji na baada ya hapo sasa tutafute masoko ya uhakika ikiwemo kuingiza hili zao katika Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, lakini baada ya kuongeza uzalishaji kwa wingi.
Name
Moshi Selemani Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tanganyika
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga soko la kimataifa la mazao ya kilimo katika eneo la Majimoto, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi?
Supplementary Question 4
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Serikali ilitenga maeneo ya kujenga soko la kimataifa eneo lile la Karema, Kijiji cha Itetemya na mpaka sasa yapata miaka mitano eneo hilo halijaendelezwa. Ni lini mtaenda kujenga soko la kimataifa katika eneo hilo?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nimthibitishie tu kaka yangu Mheshimiwa Kakoso kwamba mpango wa Serikali kujenga Soko la Karema uko palepale. Tulikuwa na changamoto ya fedha na fedha inatafutwa ili tuanze huo ujenzi.
Name
Rebeca Sanga Nsemwa
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga soko la kimataifa la mazao ya kilimo katika eneo la Majimoto, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi?
Supplementary Question 5
MHE. REBECA S. NSEMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, wananchi wa Wilaya ya Makete ni wazalishaji wakubwa wa zao la ngano. Licha ya zao hilo kutumika kutengeneza vitafunwa mbalimbali kama mikate, maandazi na chapati, lakini zao hili katika Wilaya ya Makete hutumika pia kupikia ugali ambao ni chakula kikuu kwa wananchi wengi wa Tanzania.
Je, ni lini Serikali itaweza kuwatafutia masoko wananchi hawa ili zao hili liuzwe kwa bei ambayo itaweza kuwanufaisha wakulima?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimthibitishie tu dada yangu Mheshimiwa Rebeca Nsemwa kwamba soko la ngano nchini, ndiyo ninaweza nikasema ni soko la uhakika kwa sababu ngano tunaagiza, ninaweza nikasema karibu 100% kutoka nje ya nchi. Pia tunatumia fedha nyingi sana kwa mwaka, zaidi ya shilingi bilioni 400 kuagiza ngano kutoka nje ya nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hilo ni soko la uhakika na moja ya mkakati wa Wizara (Serikali), ni kuhakikisha zao la ngano ndiyo linapewa kipaumbele. Katika hizo jitihada tunazofanya ni pamoja na Halmashauri ya Makete, Mbunge wa Jimbo hapa anafahamu, kila mwaka tumekuwa tukipeleka mbegu za ruzuku bure ili kuli-boost hilo zao. Tunaamini tukishaongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa, maana yake itatusaidia kupunguza ile tunasema gap ya uagizaji wa ngano kutoka nje ya nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, soko letu hapa nchini ni la uhakika na tutaingia katika kilimo cha mkataba ili kuhakikisha wale wananchi wanapokuwa wanalima, wanauza moja kwa moja kwa wadau, ahsante.
Name
Enock Zadock Koola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga soko la kimataifa la mazao ya kilimo katika eneo la Majimoto, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi?
Supplementary Question 6
MHE. ENOCK Z. KOOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kwenye ziara ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Naibu Waziri aliahidi kuwa soko la kisasa litajengwa Jimbo la Vunjo, Kata ya Makuyuni. Je, lini hiyo kauli au ahadi itatimizwa? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze Mheshimiwa Koola, Mbunge wa Vunjo, ni kweli kauli hiyo tuliitoa na tuna uhakika hilo soko tutalijenga, tunachokifanya sasa hivi ni kutafuta fedha ili tuanze ujenzi katika eneo hilo.
Name
Lucy Edward Mwakyembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga soko la kimataifa la mazao ya kilimo katika eneo la Majimoto, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi?
Supplementary Question 7
MHE. LUCY EDWARD MWAKYEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili kuuliza swali la nyongeza.
Kwa kuwa Serikali inajenga masoko katika maeneo mbalimbali ya kimataifa, je, Serikali ina mpango gani ili kuweka mkakati katika baadhi ya mikoa kuweza kulima kilimo cha matunda kama kilimo cha biashara ili kuwatafutia soko nje ya nchi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge Lucy Mwakyembe, mkakati wa Serikali tuna mazao ya kimkakati ya kibiashara, tuna mazao ya chakula. Hata hivyo, tumejikita sasa hivi vilevile kuhakikisha kwamba tunahamasisha mazao ya matunda katika maeneo mbalimbali na ndiyo maana utaona hata mikoa kama Mwanza maeneo ya Ukerewe tunahimiza watu kuongeza uzalishaji wa machungwa, ukienda kwenye parachichi utaona watu Mikoa ya Njombe inalimwa sana, yote tu ni katika kuhamasisha kwamba uzalishaji wa mazao ya matunda utumike kama sehemu ya mazao ya kibiashara ambayo yatasaidia kuongeza kipato cha mkulima. Kwa hiyo, ipo na ni makakati wa Serikali.