Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 39 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 465 2026-05-29

Name

Dr. Regina Christopher Malima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI K.n.y. MHE. DKT. REGINA C. MALIMA aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza kilimo cha machungwa kama mbadala wa kiuchumi Kisiwa cha Ukerewe?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, halmashauri inalo eneo linalofaa kwa kilimo lenye ukubwa wa hekta 39,121.6 ambapo malengo ya kilimo cha machungwa msimu wa mwaka 2025/2026 ni hekta 1,731.7 eneo lililolimwa mpaka sasa ni hekta 1,312 sawa na 76% ya lengo, eneo linalovunwa ni hekta 1,123 ambapo mavuno yaliyopatikana hadi sasa ni tani 37,075.5 za machungwa na uvunaji unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Serikali kupitia Halmashauri ya Ukerewe inatenga bajeti ya shilingi 30,000,000 kila mwaka kwa ajili ya ununuzi wa miche ya matunda na kuimarisha vitalu vya kuhifadhia miche. Katika msimu wa mwaka 2025/2026 halmashauri hiyo imenunua jumla ya miche 2,000 kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwa kutumia fedha za mapato ya ndani. Miche hiyo ilisambazwa kwa baadhi ya wakulima na taasisi 14 kwa ajili ya kupandwa. Aidha, Serikali itaongeza wataalamu watakaotoa elimu bora juu ya kilimo cha machungwa, kutafuta masoko na kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba hayo.