Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI K.n.y. MHE. DKT. REGINA C. MALIMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza kilimo cha machungwa kama mbadala wa kiuchumi Kisiwa cha Ukerewe?

Supplementary Question 1

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, kwa kuwa zao hili la machungwa Wilayani Ukerewe kwa sasa linalimwa kwa wingi, Serikali inaonaje kutafuta wawekezaji watakaowekeza kwenye kiwanda cha kuchakata zao hili ili kupata zao litakalokuwa na thamani zaidi? Swali la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa pia mazao haya mbadala yapo na yameenea maeneo yetu mbalimbali nchini na Jimbo langu la Maswa Magharibi tuna zao mbadala la alizeti; Serikali ina mkakati gani kutusaidia kupunguza bei ya mbegu za alizeti, lakini pia kutafuta soko la mafuta ya alizeti kutoka Wilayani kwetu Maswa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninamshukuru Mheshimiwa Mashimba Ndaki, Mbunge wa Maswa Magharibi kwa maswali mawili ya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza ni kuhusu eneo la Ukerewe ambapo ameomba jitihada za Serikali kuhakikisha tunapeleka wawekezaji na sasa hivi moja ya mchakato tulionao Wizara ni kuongea na wale wawekezaji wanaozalisha vinjwaji vinavyotokana na matunda hapa nchini huenda kama vile wale kina Jambo, watu wakina Bakhresa ambao ni Azam, kina Azania, wakina MO wote wale tumekubaliana kwamba tukae nao na tutengeneze mkakati wa pamoja wa kuhakikisha kwamba wananunua matunda hapa nchini na kusaidia wakulima wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kuhusu bei ya mbegu za alizeti, alizeti ni moja ya zao ambalo Serikali tunatoa ruzuku kwenye mbegu za zao la alizeti, kwa hiyo, ipo na tunachokifanya tu ni kuongeza idadi ya mbegu ambazo zitawafikia wakulima. Kwa hiyo, hilo nikuthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumeweka ruzuku katika alizeti na Maswa Magharibi ni sehemu ya wanufaika na tutawafikishia mbegu hizo kwa wakati.

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI K.n.y. MHE. DKT. REGINA C. MALIMA aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza kilimo cha machungwa kama mbadala wa kiuchumi Kisiwa cha Ukerewe?

Supplementary Question 2

MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni haja ya kuweka soko la kuuzia mazao yanayoharibika haraka kama vile maembe katika Mikoa yetu ya Mtwara na Lindi badala ya wanaokwenda kununua kwenda kule mashambani?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda nimtaarifu tu Mheshimiwa Mbunge dada yangu Mheshimiwa Agnes Hokororo, mkakati wa Serikali sasa hivi ni kuhakikisha kwamba tunajenga tunasema hizi cold chain facilities maeneo ambayo yanaweza kuhifadhi matunda kama maembe na machungwa katika maeneo ya mipakani kwenye border zetu ambapo mazao yanapita kutoka eneo moja kwenda lingine, lakini vilevile katika viwanja vya ndege na stesheni zetu ikiwepo SGR, huu ndiyo mpango tulionao Serikali ili kuhakikisha kwamba tunapunguza upotevu wa mzao yanayotokana na matunda.