Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 39 Water and Irrigation Wizara ya Maji 467 2026-05-29

Name

Dr. Jasson Samson Rweikiza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: -

Je, lini huduma ya maji itafika kwenye Kata za Maruku na Kanyengereko?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Jasson Samson Rweikiza, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha awamu ya kwanza na ya pili ya mradi mkubwa wa maji wa Kemondo - Maruku kwa kutumia maji ya Ziwa Victoria ambapo zaidi ya kaya 1,000 na wananchi 36,150 wa Vijiji vya Rwagati, Kanazi, Katoju, Buganguzi na Minazi vilivyopo Wilaya ya Bukoba, Mkoani Kagera vimeanza kunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awamu ya tatu ya mradi huo itaanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo itahusisha ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 500,000, ujenzi wa nyumba ya mitambo ya kusukuma maji (booster station), ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa kilometa 90.8, ujenzi wa vituo 119 vya kuchotea maji pamoja na maunganisho ya maji kwa kaya 550 zilizopo Vijiji vya Kata za Maruku, Kanyengereko na baadhi ya maeneo ya Kata ya Katerero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuboresha zaidi huduma ya maji kwenye vijiji hivyo, Serikali inaendelea na mradi wa ukarabati wa miundombinu ya usambazaji maji pamoja na chanzo cha Kiholelo katika Vijiji vya Maruku na Kanyengereko kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 492. Mradi huo umefikia wastani wa 75% za utekelezaji ambapo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka wa fedha 2026/2027.