Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Jasson Samson Rweikiza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: - Je, lini huduma ya maji itafika kwenye Kata za Maruku na Kanyengereko?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri sana ya kutia moyo kwa wananchi wa Vijiji vya Maruku na Kanyangereko. Ni kweli nimeona kwenye bajeti ya juzi hapa ya Wizara ya Maji, mradi huu umetengewa fedha kwa ajili ya kutekelezwa. Ninaishukuru Serikali kwa hatua hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina swali moja la nyongeza; Mheshimiwa Naibu Waziri mradi huu ni muhimu sana Kanyangereko na Maruku. Je, unaweza kunihakikishia kwamba mradi utapewa kipaumbele cha kwanza kwa sababu umekaa miaka sita karibu saba tangu uanze kutekelezwa na haujakamilika?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Jasson Samson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Rweikiza kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya katika Jimbo lake la Bukoba Vijijini. Ninatambua wakati akiingia madarakani upatikanaji wa huduma ya maji ulikuwa hafifu na sasa umefikia 75%. Ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge na mimi nimepata fursa ya kutembelea jimbo lile kwa mara tatu. Ninaamini kwamba kazi kubwa iliyofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inaanza kuonekana kwa vitendo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimtoe hofu na kwamba Serikali inaongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan haitapima mafanikio ya sekta ya maji kwa idadi ya miradi iliyoanzishwa, bali kwa idadi ya miradi iliyokamilika na kugusa wananchi moja kwa moja. Hivyo, hakuna mradi wa kimkakati utakaobaki kuwa kiporo. Ninataka kutumia fursa hii kumhakikishia Mheshimiwa Dkt. Rweikiza kuwa mradi wake wa Kemondo ni wa kimkakati katika Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo basi, tumehakikisha na tunahakikisha kwamba Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan itauweka katika kipaumbele cha kwanza kabisa katika kuutekeleza na ndiyo maana tumeuingiza kwenye bajeti ya mwaka huu ili awamu hii ya tatu baada ya awamu ya kwanza na ya pili kukamilika na hii ya tatu tunaenda kuikamilisha kama ilivyo maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ahsante sana.

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: - Je, lini huduma ya maji itafika kwenye Kata za Maruku na Kanyengereko?

Supplementary Question 2

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kumekuwa na shida kubwa sana ya maji katika Kata ya Ramadhani, maeneo ya Mgendela na Njombe Mjini; Kata ya Kitisi, Jimbo la Makambako na Kata ya Wanging'ombe, Kijiji cha Katenga na Mbembe Jimbo la Wanging'ombe. Je, lini Serikali itamaliza shida hii ya maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Neema Mgaya, Mbunge Viti Maalum Njombe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana kwa kazi kubwa ya kuwatetea akinamama na kwa ushirikiano mkubwa anaowapatia Waheshimiwa Wabunge ukiwemo Mheshimiwa Mwenyekiti. Nimtoe hofu, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inao mradi mkubwa sana umewekezwa Njombe, Makambako mpaka Wanging'ombe una gharama ya shilingi bilioni 125.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo tunaamini kwamba mradi huu ukishakamilika basi utaweza kutoa huduma huduma iliyotarajiwa kwa wananchi na iwapo kutakuwa na maeneo ambayo yatabaki na changamoto, tunayo programu maalumu ya vijiji 1,575 napo tutahakikisha kwamba tunaanza kuingiza kijiji kimoja baada ya kingine. Lengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 vijiji vyote vitakuwa vimepata huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana.

Name

Agnesta Lambert Kaiza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: - Je, lini huduma ya maji itafika kwenye Kata za Maruku na Kanyengereko?

Supplementary Question 3

MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi. Mheshimiwa Naibu Waziri utakubaliana na mimi kwamba pamoja na jitihada kubwa na nzuri zinazofanyika ndani ya Jimbo la Segerea kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama, jitihada hizi hazijaleta matokeo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana Serikali kwa kuliona hilo ikaagiza pampu nne. Pampu ambazo zikija kufungwa Mto Ruvu, wananchi wa Jimbo la Segerea pamoja na wakazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam watakwenda kuondokana na adha hii kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu; ninatambua pampu tayari zilikwishakufika. Je, zoezi la kufunga pampu hizi limefikia wapi na ni lini mradi huu utakamilika ili wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam waweze kupata maji safi na salama?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Segerea, kwanza kwa ufuatiliaji na kwa kujua hatua kwa hatua sekta ya maji inavyofanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni dhahiri na ni ishara tosha ya kuonesha kwamba Serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inafanya mambo yake kwa uwazi na kwa kushirikiana na ndiyo maana tumefikia katika hatua ya kuona Mheshimiwa Mbunge anakuwa anajua chain yote ya mchakato. Nikutoe hofu kazi kubwa ilikuwa kununua hizo pampu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi iliyobaki na kwa wataalamu tulionao ndani ya sekta ya maji ninakuhakikishia kwamba hizo pampu tunaenda kuzifunga na wananchi wako wa Jimbo la Segerea wakapate huduma ya maji safi na salama na mradi huo utakuwa umeanza kutoa huduma inayotarajiwa kwa wananchi. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Kijakazi Mohamed Yunus

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: - Je, lini huduma ya maji itafika kwenye Kata za Maruku na Kanyengereko?

Supplementary Question 4

MHE. KIJAKAZI Y. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona ili niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Kata Lihimalyao, Wilayani Kilwa hususan akinamama wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu. Maji ambayo yamekuwa yakipatikana pale ni maji ya chumvi kali sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iliahidi kuleta maji kutoka kata jirani kwa kupitia Mradi wa Pande Plot. Ningetamani kufahamu ni upi mpango wa Serikali au Serikali imejiandaaje kutekeleza ahadi ile ili kuweza kuikata kiu ya Mheshimiwa Rais ya kuhakikisha kila mwanamke tunamtua ndoo kichwani? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kijakazi Mohamed, Binti Lindi, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Lindi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya na sisi sekta ya maji tunamwahidi ushirikiano kuhakikisha kwamba anatimiza falsafa ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatambua na Serikali inafahamu Lihimalyao ni eneo ambalo kweli maji yake hata kama ukitumia gharama yoyote ya kuyatibu matokeo yake maji yatafika kwa watumiaji yakiwa na changamoto ya gharama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunachokwenda kukifanya tunakwenda kuchukua maji kutoka Pande Plot ambapo Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluh Hassan kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo tumepata KfW ambao wamekubali kushirikiana nasi kwenda kuyatoa katika Kata ya Pande ambapo ya Pande haya ni maji safi na salama, hayana changamoto ya chumvi ili kuhakikisha kwamba wananchi wa Kata Lihimalyao wanapata huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana.

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: - Je, lini huduma ya maji itafika kwenye Kata za Maruku na Kanyengereko?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Lyamidati iliyoko katika Jimbo la Solwa, maji ya Ziwa Victoria yamepita kwenye miji ya watu, yale mabomba yamepita kwenye mji wa mtu, lakini wananchi wale hawana maji. Nini kauli ya Serikali kuhusu wananchi hawa ambao wanalinda miundombinu, lakini maji hawana? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Christina Mnzava, Mbunge Viti Maalum kutoka Mkoa wa Shinyanga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba bomba limepita katika makazi ya watu na linapita katika Jimbo la Solwa, lakini pia linapita katika Jimbo la Itwangi ambapo changamoto ni hiyo hiyo, lakini Serikali tumeliona hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa tumeweka bajeti ya kwenda kuanza na baadhi ya vijiji ili tuhakikishe kwamba wanapata huduma ya maji safi sana na salama, lakini katika bajeti zijazo tutaendelea kutenga fedha ili kuhakikisha kwamba wananchi hao wanaendelea kunufaika na maji ambayo kimsingi wamejitolea maeneo yao na mabomba yamepita hapo. Kwa namna nyingine tunasema kwamba mradi huo wameufanya kuwa wao na sisi Serikali tutahakikisha kwamba tunazingatia hilo ili wapate huduma ya maji safi na salama. Ahsante sana.